KUFANYA MAZOEZI NA KULA DIET TU SI MATOKEO YA MUHIMU YA KUWA NA AFYA BORA YA UJUMLA YA MWILI NA AKILI
Kwa maendelea tuliyonayo kwa sasa tumefikia kujua vitu kadhaa kwa maarifa yetu pengine vinaweza kutupa afya ya mwili kama tukivifanya ipasavyo. Tunahisi tunaweza tukawa bora zaidi kuhudumia mwili kuliko wakati uliopota. Afya imetafsiriwa kwa upana sana na lengo ni kufikia kupata mwili wenye afya bora.
Tumeanzisha njia za maisha kwa kubadilisha kula, kulala vizuri na mazoezi kama mbinu za kufikia afya bora ya mwili. Kila mtu anahangaikia vitu hivyo na mara nyingi vinasikika masikioni mwetu na kuona. Imeshakuwa ni staili yetu ya maisha na kuhamasishana.
Tukiangalia kwenye maisha yetu licha ya kutimiza vyote hivyo kula vizuri, mazoezi na kulala muda sahihi bado afya yetu haiko sawa kuna kitu tunachokikosa na ni cha muhimu sana. Tutafanya vyote tunavyo vijua lakini ukiangalia kwa makini ni kama tunapoteza nguvu zetu na kujichosha tu. Inachopelekea tunajidhuru zaidi kwa jina la kujipa afya na kubaki kutopata faida yoyote.
Kitu tunachokikosa ni kipi, ni fumbo gani tunaloshindwa kulifumbua tukapata faida ya afya bora kwenye ubinadamu wetu. Tumesahau akili ina muunganiko na mwili wa karibu sana na huwa hatujali ubora wake wakati tunapigania kupata afya ya mwili. Kusahau hili ni kama unajenga nyumba bila kuwa na msingi ni muda wowote inadondoka.
Ina maana gani ubora wa akili kwenye afya ya mwili. Miitikio yoyote inayotokana na akili kutokuwa sawa ina madhara makubwa ya kuharibu mwili kuliko nguvu zako zote na mbinu unazojua zakukupa afya bora. Mawazo ya mtu yana nguvu ya kufikia kumuangamiza mwenyewe bila kuwa na kichocheo kutoka nnje. Afya ya akili ni kitu cha kwanza kwenye ubora wa mtu kabla ya mbinu yoyote ile unayoweza kuitumia.
Ubora wa akili wakijitambua na kutojidhuru mwenyewe kwa kutofanya hisia na mawazo kuwa chanzo cha woga, wasi wasi, kutojithamini, huzuni, mzio na mengi zaidi tunayozalisha akilini mwetu na kutoa furaha yetu yote ya maisha na kutupa kuchanganyikiwa kunakotudhuru zaidi ya tunavyoweza kufikiri.
Nb: Ufahamu wa kujitambua na kuweza kujua undani wetu ni njia bora ya kutupa afya ya kudumu ya mwili na akili na si kujitesa na kujinyima kama njia ya kupata mafanikio ya afya bora huku akili zetu zikiwa na sumu kubwa inayotuangamiza.
Fungua link kujifunza zaidi,
https://lastphilos.wixsite.com/psyche/post/kufanya-mazoezi-na-kula-diet-tu-si-matokeo-ya-muhimu-ya-kuwa-na-afya-bora-ya-ujumla-ya-mwili-na-aki