• Call us +255 717 568 861

Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Endeleza Kipaji Chako - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

ENDELEZA KIPAJI CHAKO

Ratings

Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Num added to cart:
0
Added to shop:
Jul 31, 2020
In category:
Sample

Jinsi Ya Kuendeleza Kipaji Ulicho Nacho Na Kuleta Tofauti Katika Maisha Yako.

       Endeleza kipaji chako ni mwendelezo wa pili baada ya kitabu cha  kwanza cha “Gundua kipaji chako” ambacho kimefanyika baraka kubwa katika kuwasaidia watu kugundua vipaji vyao. Ili Kipaji kiweze kuleta matokeo katika maisha ya mtu, haitoshi tu kukigundua na kukitambua, ni lazima kiendelezwe au kinolewe. Kipaji kisichotumika na kuendelezwa hudumaa na kuwa butu. Kugundua kipaji chako ni hatua moja na kuendeleza kipaji chako ni hatua nyingine.

 

Kanuni ya Ki-mungu ni kwamba kadri unavyotumia uwezo wako ndivyo unavyoongezeka. Kuendeleza vipaji vyako kunachukua muda na juhudi sawa na namna ile ulivyojifunza kusoma, kuandika na kutembea. Usijikatie tamaa mwenyewe hasa unapofikiri huoni matokeo yoyote chanya. Vipaji vingine vinahitaji juhudi zaidi katika kuviendeleza kuliko vingine.

 

Elizabeth Hand alisema maneno haya , “ Kipaji usipokitia moyo, na usipokifunza, kitakufa. Kinaweza kukimbia kwa fujo kwa kitambo tu, lakini haitakuwa na maana yoyote. Ni kama farasi mwitu. Kama usipomfuga na kumfundisha kukimbia katika njia, kupima mwendo wake, na njinsi kumbeba mwendeshaji, haijalishi anakimbia kiasi gani. Farasi huyo hafai.” 

Katika kitabu hiki utapa kujifunza juu ya nguvu ya kipaji chako, Namna unavyoweza kuendeleza kipaji chako, Vile unavyoweza kuvishinda vizuizi vya katika kuendeleza kipaji chako, lakini pia utajifunza namna gani uweze kuchochea na kung’arisha kipaji chako  na faida utazapota kwa kutumia kipaji chako.

Other products from this category