Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Malezi Katika Msingi Imara - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

MALEZI KATIKA MSINGI IMARA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
5,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Dec 04, 2021
Product Views:
275
In category:
Sample

NENO LA UTANGULIZI BISHOP DICKSON D. KAGANGA: TAG ZANZIBAR Wataalam wa maandishi (literature) wanatuambia kuwa waweza kumjua mtu kwa kusoma maandishi yake. Kitabu hiki "Malezi Katika Msingi Imara," kinamweleza mwandishi (shauku yake, mzigo wake, na hata vile yeye mwenyewe alivyo - mcha Mungu anayeweka maadili ya kiroho katika malezi kuwa ni kipaumbele). Kitabu hiki, kinamweleza mwandishi (James Mwalubalile), kuwa yeye mwenyewe amelelewa katika nyumba ya namna gani (nyumba ya kiroho na aliyepata "Malezi yenye msingi imara," hata kabla hajaandika juu ya "Malezi Katika Msingi Imara"). Nafikiri sote tutakubaliana kuwa kuna changamoto kubwa katika suala zima la kulea watoto. Mtoto anapozaliwa kunakuwa na furaha na matumaini makubwa kwa wazazi (baba na mama). Kwa bahati mbaya sana baadhi wameshuhudia furaha na matumaini hayo yakififia kadiri mtoto anapozidi kukua. Mtoto aliyetarajiwa kuendelea kuwa sababu ya furaha na matumaini kwa wazazi ghafla anageuka na kuwa sababu ya uchungu na huzuni kwa wazazi: • Anakataa kwenda shule • Anakataa kwenda Kanisani • Anakataa maelekezo ya wazazi na hata kukimbia nyumbani • Anaanza hata kuvuta sigara, bangi, bombe, madawa, na kuiba • Anapata mimba zisizotarajiwa nje ya ndoa, nk. Haya mambo na mengineyo yanayofanana na haya ambayo sikuyataja hapa huleta uchungu, simanzi, na huzuni kubwa kwa wazazi. Hufifisha ile furaha na matumaini ya baba na mama aliyokuwa nayo kwa mtoto wake. Ni kama ndoto yao inazimwa kwa upesi sana. Lakini tatizo ni nini hasa? Nini chanzo cha mabadiliko haya tusiyoyataka wala kuyatarajia kwa watoto wetu? Moja kati ya sababu ni MALEZI. Malezi, kama alivoeleza mwandishi ni msingi wa jengo liitwalo "MAISHA." Msingi usipokuwa imara jengo haliwezi kuwa imara. Kitabu hiki, ni moja kati ya vitabu vichache nilivyovisoma ambavyo vimeandikwa kutoka MOYONI na siyo kutoka KICHWANI. • Ni kitabu kilichoandikwa na mtu anayeamini kile anachokiandika. • Ni kitabu kinachofaa kusomwa na WAZAZI wa sasa (wenye watoto) na wazazi WATARAJIWA (wale watakaokuwa na watoto baadaye). • Ni kitabu kinachofaa kusomwa na WAUMINI na hata wasio waumini ambao wangetamani wawalee watoto wao kuelekea hatima iliyo bora na yenye manufaa. Kitabu hiki chafaa kutumika na waalimu wetu wa WATOTO kwani kimeandikwa katika namna ambayo chaweza kutumika kama kitabu cha kiada. Hakika ni kweli kabisa kuwa "Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataicha hata atakapokua mzee" (Mithali 22:6). Bishop Dickson D. Kaganga (BA, MA, Mdiv, Dmin - candidate

NENO LA UTANGULIZI

BISHOP DICKSON D. KAGANGA: TAG ZANZIBAR

Wataalam wa maandishi (literature) wanatuambia kuwa waweza kumjua mtu kwa kusoma maandishi yake. Kitabu hiki "Malezi Katika Msingi Imara," kinamweleza mwandishi (shauku yake, mzigo wake, na hata vile yeye mwenyewe alivyo - mcha Mungu anayeweka maadili ya kiroho katika malezi kuwa ni kipaumbele). Kitabu hiki, kinamweleza mwandishi (James Mwalubalile), kuwa yeye mwenyewe amelelewa katika nyumba ya namna gani (nyumba ya kiroho na aliyepata "Malezi yenye msingi imara," hata kabla hajaandika juu ya "Malezi Katika Msingi Imara").

Nafikiri sote tutakubaliana kuwa kuna changamoto kubwa katika suala zima la kulea watoto. Mtoto anapozaliwa kunakuwa na furaha na matumaini makubwa kwa wazazi (baba na mama). Kwa bahati mbaya sana baadhi wameshuhudia furaha na matumaini hayo yakififia kadiri mtoto anapozidi kukua. Mtoto aliyetarajiwa kuendelea kuwa sababu ya furaha na matumaini kwa wazazi ghafla anageuka na kuwa sababu ya uchungu na huzuni kwa wazazi:

•          Anakataa kwenda shule

•          Anakataa kwenda Kanisani

•          Anakataa maelekezo ya wazazi na hata kukimbia nyumbani

•          Anaanza hata kuvuta sigara, bangi, bombe, madawa, na kuiba

•          Anapata mimba zisizotarajiwa nje ya ndoa, nk.

Haya mambo na mengineyo yanayofanana na haya ambayo sikuyataja hapa huleta uchungu, simanzi, na huzuni kubwa kwa wazazi. Hufifisha ile furaha na matumaini ya baba na mama aliyokuwa nayo kwa mtoto wake. Ni kama ndoto yao inazimwa kwa upesi sana.

Lakini tatizo ni nini hasa? Nini chanzo cha mabadiliko haya tusiyoyataka wala kuyatarajia kwa watoto wetu? Moja kati ya sababu ni MALEZI. Malezi, kama alivoeleza mwandishi ni msingi wa jengo liitwalo "MAISHA." Msingi usipokuwa imara jengo haliwezi kuwa imara.

Kitabu hiki, ni moja kati ya vitabu vichache nilivyovisoma ambavyo vimeandikwa kutoka MOYONI na siyo kutoka KICHWANI.

•          Ni kitabu kilichoandikwa na mtu anayeamini kile anachokiandika.

•          Ni kitabu kinachofaa kusomwa na WAZAZI wa sasa (wenye watoto) na wazazi WATARAJIWA (wale watakaokuwa na watoto baadaye).

•          Ni kitabu kinachofaa kusomwa na WAUMINI na hata wasio waumini ambao wangetamani wawalee watoto wao kuelekea hatima iliyo bora na yenye manufaa.

 Kitabu hiki chafaa kutumika na waalimu wetu wa WATOTO kwani kimeandikwa katika namna ambayo chaweza kutumika kama kitabu cha kiada.

Hakika ni kweli kabisa kuwa "Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataicha hata atakapokua mzee" (Mithali 22:6).

 

Bishop Dickson D. Kaganga (BA, MA, Mdiv, Dmin - candidate

More Products On Discount
10,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

Best Sellers List
Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

Best Seller
25,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PIUS JUSTUS

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
1,000 Tsh.

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold