-
+255 717 568 861

SIRI ZA BIASHARA KWA AJILI YA KUZIDISHA MAPATO
Ratings
Kitabu Pekee Kinachokupatia Mwongozo Kamili Wa Kukuza Biashara -- Zungumza LughaMoja Na Wateja! Tengeneza Masoko! Zidisha Mapato! Na Kuza Biashara Yako Upesi Kuliko Ushindani! Nunua Kitabu Hiki Na Utapata...
Mwongozo wa Njia-7 Kwa Ajili Ya Kuzidisha Mapato!
Watu wengi wanateseka kukuza biashara bila mwongozo
wowote. Haiwezekani kutimiza malengo yetu ya kibiashara, ikiwa tutaendelea kutafuta
wateja huku na kule kama mtu anayefukuza upepo. Kitabu cha SIRI ZA BIASHARA
kinatatua tatizo hili kwa kuwapatia wasomaji “NJIA-7 ZA KUTANUA MASOKO.” Huu ni
mwongozo kamili wa kupata wateja na kukuza biashara.
Baadhi ya mambo utakayojifunza katika kitabu hiki ni
pamoja na:
- Siri
ya kuzungumza LughaMoja na wateja [Ndiyo! Bila kuwaeleza wateja kwanini
wanunue bidhaa zako, watakupuuza wewe na biashara yako. Hili ndiyo tatizo
namba moja ambalo kitabu hiki kinatatua. Lakini pia, utajifunza:
- Kanuni
ya kutumia “NGUVU YA MANENO” kupata kitu chochote unachotaka bila
kukataliwa na mtu yeyote
- Maswali
19 ambayo kila mmiliki wa biashara anatakiwa kujibu kwa ufasaha [Hii ndiyo
siri ambayo wenzetu wanatumia kutengeneza makampuni yenye nguvu]
- Biashara
yako ingekuwa mtoto, ungeipatia uji wa wa lishe au makande? Jibu lipo
ndani ya kitabu hiki cha SIRI ZA BIASHARA
- Kosa namba #1 ambalo watu wengi wanafanya wanapojaribu kuuza bidhaa
- Hatua tatu muhimu katika UKUAJI WA BIASHARA. Unazijua?!
- VITU VITANO unavyohitaji kuvijua vizuri kabla ya kuingiza bidhaa sokoni
- Mbinu saba za kulenga soko [Ulengajisoko ni sanaa mpya ambayo itakusaidia kupata wateja wenye tija na hivyo kuzidisha mapato yako ya biashara]
- Siri
ya kumfanya mteja kuzipenda bidhaa zako kama vile ana hisa
- Fomla
ya kupata wateja bila kufanya matangazo ya biashara
- Na
siri nyingine nyingi ambazo hujawahi kuzisikia mahali popote hapa duniani. [Hujawahi kuzisikia siyo kwa sababu ni mvivu kusoma, la hasha!] Siri hizi zimefichuliwa katika kitabu hiki
kwa mara ya kwanza. Kwa hiyo, usikubali washindani wazipate silaha hizi za mafanikio
kabla yako.
Unataka kujifunza mbinu ambazo makampuni makubwa
yanatumia kutawala soko? Ndani ya kitabu hiki Vianney Mahimbi amedhihirisha
ubingwa wake wa kutengeneza miundo ya biashara, mifumo ya masoko, mbinu za kuzidisha
mapato na vifaa ambavyo kila mmiliki wa biashara anahitaji ili kukua na kustawi
katika karne ya 21.
Kwa hiyo, kama wewe ni mmiliki wa biashara, mjasiriamali, mkurugenzi wa mashirika ya kijamii au unataka kutumia nguvu ya biashara kufanikisha malengo yako. Kitabu cha SIRI ZA BIASHARA kitakupatia mwongozo wa kupata wateja, kutanua masoko na kuzidisha mapato. Na uzuri ni kwamba, mwongozo huu wa Njia-7 umerahisishwa katika ukurasa mmoja.
Nunua SIRI ZA BIASHARA KWA AJILI YA KUZIDISHA MAPATO kwa kubofya batani iliyoandikwa Buy now