Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Tatizo Si Rasilimali Zilizopotea - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 01, 2020
Product Views:
1,744
In category:
Sample

Tatizo ni RasilimaliWatu Tunaowapoteza

Kwa siku nyingi sasa kumekuwepo na malalamishi kutoka kwa watu mbalimbali, ndani na nje ya bara la la AFRIKA, malalamishi haya haswa yanaelekezwa kwa wazungu na wakoloni na watu nchi za nje. Watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba sasa bara la Afrika lingekuwa limepiga hatua kubwa sana kama wasingekuwa wakoloni waliotawala nchi hizi za Afrika na kuchukua rasilimali nyingi sana. Katika kitabu hiki utakutana na mtazamo wa tofauti kutoka kwa mwandishi. Mwandishi atakuonesha kwamba rasilimali zilizopotea si tatizo kama ambavyo watu wengi wanafikiri. Hii ni kutokana na ukweli kwamba rasilimali bado zinazidi kupotea mpaka sasa hivi. Kila mtu ni shuhuda juu ya madini, wanyamapori na mchanga ambao umekuwa ukizidi kubebwa na kupelekwa nje ya nchi kila mwaka, ingawa wakoloni hawapo.

Si hilo tu bali watanzania na waafrika kwa ujumla wamezidi kuwa nyuma kwa mambo mengi ikiwemo mambo ya uwekezaji, uhuru wa kiuchumi, sayansi, utafiti kutaja ila machache.

Hii ni kutokana na imani ya watu wengi ambao wanaamini kwamba mwekezaji ni mtu kutoka nje ya nchi na wengine wanaamini kwamba vitu vingine si vya viwango vyao bali vinastahili kufanywa na wazungu. Basi kwa hali hii bila shaka utakubaliana na mimi kwamba TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA.

Sasa kama tatizo si raslimali zilizopotea tatizo ni nini?

Katika kitabu hiki utapata kujifunza kwamba rasilimali watu zinazopotea sasa hivi. Kwa sasa tunazipoteza rasilimaliwatu kwa njia nyingi sana. Hii ni kutokana na watu wengi kutokujua kwamba wanao uwezo mkubwa sana ndani yao ambao wanapaswa kuutumia ili uwatoe sifuri mpaka kileleni. Njia hizo zinazosababisha tupoteze rasilimali watu, sasa zimeelezwa ndani ya kurasa za kiabu hiki.

 

Vijana sasa wanashinda katika vijiwe vya zama za taarifa ambayo ni mitandao ya kijamii kama wasapu, instagram, twitter, na facebook. Vijana wanapoteza muda mwingi kujadili vitu ambavyo havina manufaa kwao na kwa jamii yetu. Vijana wengi wanaamini kwamba mtu fulani ambaye yuko sehemu fulani katika nchi fulani ndiye anayehusika na kufanikiwa kwao. Ndio maana muda mwingi sana unawakuta mtandaoni wakipoteza muda kwa kujadili vitu ambavyo havina maana. Wanalamikia serikali juu ya ajira. Lakini vijana hao hao unawakuta wanazurura mtaa mmoja mpaka mwingine.

 Wanazurura kutoka kwa mjomba kwenda kwa shangazi mara kwa bibi, mara kwa babu upande wa mama kizaa mama. Wanazurura kwa kisingizio cha kwamba  hawana ajira au kisingizio cha ninatafuta ajira.

Lakini hata hivyo wale wanaowapokea nao wanazidi kusababisha tupoteze rasilimali muhimu ambazo zingeweza kuanzisha kitu.  Rasilimali ambazo zimesubiriwa zina mziki ndani yao, rasilimali zenye viwanda katika fikra zao.

Kila mtu kazaliwa akiwa mshindi, na kila mtu ndani yake zimewekwa mbegu za ushindi. Maisha mazuri, utajiri, ushindi, mahusiano mazuri, amani, kazi nzuri na biashara iliyofanikiwa. Vyote hivi ni haki ya kuzaliwa ya kila mtu. Lakini kuzaliwa ukiwa mshindi haitoshi. Kama haupo tayari kulipa gharama ya ushindi. Unapaswa kujua wapo unaenda na kwa nini unaenda huko.

Kila mara jiulize swalije, mimi……(weka jina lako) niko wapi? Ninafanya nini? Je, nimekuja hapa kufanya nini? Kama utajikuta hufanyi kile ambacho unapswa kufanya hata kama wewe umezaliwa mshindi, my friend, ushindi utausikia redioni. Umezaliwa mshindi lakini unapaswa kuhakikisha kwamba unalipa gharama ya ushindi na kufanya kazi kiushindi kila wakati.

 

 Kisome kitabu hiki mwanzo mpaka mwisho maana kuna mambo mengi sana ya kujifunza.  Hakika usiruke wala kutafuta sura ambazo wewe unaona kama zinakufaa. Wewe ni mtu wa muhimu sana na jamii nzima imesubiri na inataka kusikia kutoka kwako. Badili mtazamo wako ili uweze kubadili maisha yako.

Kuna uwezo mkubwa sana ndani yako ambao bado haujaufahamu na bado haujaanza kuutumia. Kama wewe ni moja ya watu ambao wangependa kuutumia uwezo huu mkubwa ulio ndani. Kama wewe ni moja ya watu ambao wangependa kuitumia dhahabu hii kubwa sana ambayo haijachomwa hata kidogo, basi kitabu hiki kinakufaa sana, kwa hakika umeshikilia hazina itakayobadili maisha yako. Badili fikra zako kwa kusoma kitabu hiki. Haitoshi tu wewe kusoma kitabu hiki na kutulia. Hatua  madhubuti zinapaswa kuchukuliwa baada ya wewe kusoma kitabu hiki. Msimamo wa mwandishi ni ule ya kwamba mtu yeyote anaweza kukuweka katika njia sahihi, lakini hawezi kukuamrisha wewe kuitembea njia hiyo. Kitabu hiki kinaonesha njia tu! Ila suala zima la kuifuata njia hiyo lipo juu yako.

Wewe Ni Zaidi Ya Ulivyo Sasa

Chukua hatua sasa

Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio!!!!

Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio!!!

Ndimi,

Godius Rweyongeza

($onga mbele)

Kocha, mjasiliamali na mwandishi

More Products On Discount
7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

10,000 Tsh.
(0.8)

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold
4,000 Tsh.

Sold by: Meinrald Mtitu

15,000 Tsh.

Sold by: IVAN MAHIMBI

1,000 Tsh.

Sold by: Jabir Khamis

3,000 Tsh.

Sold by: Muddyb Mwanaharakati