-
+255 717 568 861

Ushindi Katika Nyakati Ngumu
Ratings
UKWELI KUHUSU HALI NGUMU KATIKA MAISHA, SIRI YA USHINDI, NA JINSI YA KUKABILIANA NA UGUMU KATIKA ENEO LOLOTE LA MAISHA YAKO.
KUHUSU KITABU
"Ushindi Katika Nyakati
Ngumu" ni kitabu ambacho kitakusaidia jinsi unavyoweza kukabiliana na hali yoyote
ngumu katika maisha yako, namna ya kuiona nuru pale ambapo kila mmoja
anapoliona giza na jinsi ya kukitumia kinywa chako katika kuuandaa ushindi
dhindi ya changamoto.
Hakuna ambaye
huwa hapitii nyakati ngumu katika maisha yake, kila mmoja kwa nafasi yake na
kwa wakati wake huwa anapita katika kipindi fulani cha ugumu katika
maisha yake. Namna unavyoweza kukabiliana na kipindi hicho, ndiyo itakayo amua
ama upande zaidi katika maisha yako au ushuke zaidi. Waliofanikiwa katika
maisha huwa hawana mbinu za kuyakimbia yale magumu yanayokuja upande wao bali
wanazo mbinu za kukabiliana na magumu hayo.
Kitabu hiki ni
jibu kwa swali lile linalo uliza "Nifanye nini ili niweze kushinda
katika kipindi hiki kigumu ninachokipitia?" Kitabu hiki kimeandikwa kwa
lengo la kuwasaidia watu namna ya kuweza kuzitumia nyakati ngumu wanazozipitia
kama daraja la kuwapandisha badala ya kuwashusha.
KUHUSU MWANDISHI
Abel E Kiharo (Kaka Abel) ni kijana
aliyeokoka, mtoto wa tisa katika ndoa ya Elias Kiharo na Sarafina Balizigiye.
Kwasasa Abel ni mwanafunzi katika chuo cha Kabanga College of Health And Allied
Sciences akiwa anasomea kozi ya uafisa tabibu katika ngazi ya stashahada.
Abel ni mwandishi, mkufunzi wa vijana (Youth
trainer) na mwalimu wa Neno la Mungu mwenye kiu ya kuwaona watu wakiuishi
upekee wa maisha yao. Amekuwa akiandika kwa muda mrefu makala mbalimbali na
kuzisambaza kwa njia ya mitandao ya kijamii, ambazo zimewasaidia watu wengi
mpaka sasa katika kuuishi upekee wa maisha yao.
Pamoja na kuwa mwandishi, Abel ni mwanafunzi wa kudumu katika mahusiano, uongozi, afya na ujasiriamali. Anaamini siri ya mafanikio ya kweli katika maisha ni kuugundua, kuufurahia na kuuishi upekee wa maisha yako.