KWANINI NI MUHIMU KWA MAMA NA MWENZI WAKE KUANZA KLINIKI MAPEMA MIMBA CHINI YA WIKI 12?
Jipatie Kitabu \"Kwanini ni Muhimu Kwa Mama Na Mwenzi Wake Kuanza Kliniki Mapema Mimba Chini Ya Wiki 12?\r\nUkajifunze wewe na mwenzi wako na jamii inayokuzunguka mashauri na kanuni mbalimbali za kitaalamu kuhusu afya ya mama na mtoto.TUWAVUSHE SALAMA na hili liko ndani ya UWEZO WAKO.Pesa ya kununua kitabu hiki ni ndogo sana ukilinganisha na thamani ya elimu utakayoipata.KUMBUKA: Ukimsaidia mama mwenye viashiria vya kiafya visivyo vya kawaida au mwenye dalili za hatari wakati wa ujauzito utaokoa maisha yake na ya mtoto aliyetumboni na ukiokoa wote umeokoa jamii.
Idadi ya akina mama na wenzi wao wanaoanza kliniki kwa kuchelewa mimba zaidi ya wiki 12 inazidi kuongezeka na imepelekea wengi kuchelewa kupata huduma nyingi za kiafya ambazo wangelianza kuzipata mimba chini ya wiki 12.Ambapo wengine kwa kuchelewa huko wamejikuta wakikabiliwa na matatizo kadhaa ya kiafya wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua, matatizo ambayo mengine yanahitaji huduma za dharura.Siku za hivi karibuni kwa mfano idadi ya akina mama wenye upungufu mkubwa wa damu, mimba zinazotishia kuharibika/zinazoharibika, kifafa cha mimba, watoto wanao zaliwa wakiwa na ulemavu wa kimwili, vifo vya akina mama na watoto wachanga bado limekuwa ni tishio hapa kwetu Afrika.
Mengi ya matatizo hayo yanayozidi kutokea leo miongoni mwa akina mama wakati wa ujauzito, uchungu na kujifungua yanaweza kuzuilika.Moja ya njia bora ya kuzuia/kupunguza matatizo hiyo ni mama na mwenzi wake kuomba ushauri wa kitaalamu kabla hawajaamua kupata mtoto ikiwa kuna viashiria vya kiafya visivyo vya kawaida na kuanza kliniki mapema mimba chini ya wiki 12 na kuendelea kuhudhuria kliniki kadiri umri wa mimba unavyoongezeka kwa ajili ya uchunguzi, ushauri na matibabu.
Ukisoma kitabu hiki mpaka mwisho utajifunza yafuatayo:
- Dalili za mimba ya kawaida, mimba ya kawaida iliyo na kasoro, mimba zabibu, mimba isiyo na kiini au mimba hewa na jinsi zinavyotofautiana
- Sababu zinazopelekea kuzaliwa kwa watoto wenye kasoro za kuzaliwa(congenital abnormalities) na jinsi ya kujikinga zisitokee kwenye kizazi chako
- Kwanini akina mama wengi hawahudhurii mapema kliniki mimba chini ya wiki 12 na nini suluhisho lake
- Kwanini ni muhimu kwa mama na mwenzi wake kuanza kliniki mimba chini ya wiki 12? Faida 22 utajifunza
- Jinsi ya kukabiliana mapema na historia ya hali yoyote ya kiafya ya mama aliyonayo/aliyowahi kuwa nayo inayoweza kuathiri afya yake na mtoto tumboni
- Jinsi ya kukabiliana mapema na matatizo ya kiafya mama na mwenzi wake kabla ya ujauzito na wakati wa ujauzito
- “Ni rahisi kumpoteza mtoto kuliko mama, lakini ni rahisi zaidi kuwapoteza wote ikiwa hakuna jitihada za kitaalamu zilizofanyika kukabiliana na hali yoyote ya kiafya isiyo ya kawaida au dalili ya hatari wakati wa ujauzito .Ukimsaidia mama mwenye viashiria vya kiafya visivyo vya kawaida au mwenye dalili za hatari wakati wa ujauzito utaokoa maisha yake na ya mtoto aliyetumboni na ukiokoa wote umeokoa jamii\" Usikose nakala ya kitabu hiki.
Kupata hardcopy ya kitabu hiki lipia Sasa TSh 20,000/= Kisha tuma SMS/Piga 0686279021 ya muamala wako wa Malipo Jina Lubango Lucas Chikanda kitakufikia huko uliko kwa uaminifu mkubwa.
Nauri ya kusafirisha kitabu hiki kwa hapa Tanzania ni juu yangu.Mungu akubariki
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher