
MTU SAHIHI WA KUFANYA NAYE BIASHARA
Kitabu cha Mtu Sahihi Wa Kufanya Naye Biashara, kinakufundisha jinsi ya kuchagua mshirika wa kweli katika biashara yako.
Kama unataka kupata matokeo makubwa katika biashara yako…
Unahitaji kufanya biashara na watu sahihi. Hawa ni washirika
wa kweli ambao watakusaidia kutatua changamoto zinazokukabili na kukupatia
rasilimali unazohitaji ili kukua na kustawi katika biashara yako.
Nilipata mateso ya kisaikolojia na kushindwa kutimiza
ndoto zangu kwa sababu sikujua jinsi ya kuchagua watu sahihi wa kufanya nao
biashara. Nilizungukwa na watu ambao badala ya kunisaidia kutimiza malengo
yangu, wananirudisha nyuma. Lakini naweza kukusaidia kuepuka makosa ambayo mimi
nilifanya.
Kitabu cha Mtu
Sahihi Wa Kufanya Naye Biashara, kinakufundisha jinsi ya kuchagua mshirika
wa kweli katika biashara yako.
Ndiyo, washirika wa biashara wanaweza kukusaidia kuongeza
kipato na kufanya vitu vya maana katika jamii.
Mshirika wa kweli mmoja tu, anatosha kubadilisha maisha
yako.
Kwa hiyo, kama unataka kufika mbali katika safari ya
mafanikio…
Usiende peke yako. Kuna watu wana uzoefu na rasilimali
ambazo unahitaji ili kutimiza malengo yako.
Kitabu hiki kinakusaidia kutambua biashara yako inahitaji
nini, na kukupatia fomla ya kuchagua watu ambao watakupatia kila kitu
unachohitaji. Hawa ni watu sahihi wa kufanya nao biashara.
JIFUNZE JINSI YA KUCHAGUA WATU SAHIHI WA KUFANYA NAO
BIASHARA
Watu wanaokuzunguka wanaweza kukusaidia kujenga biashara
yako au kubomoa kila kitu.
Katika uzoefu wangu, nimegundua kwamba:
1. Kama
unashindwa kutimiza malengo yako ya biashara, ama umezungukwa na watu ambao
wanakurudisha nyuma.
2. Au,
unateseka kufanya biashara peke yako.
Lakini kuna njia nyepesi ya kufanikiwa!
Soma kitabu hiki na utaweza kuchagua MTU SAHIHI WA
KUFANYA NAYE BIASHARA na ndoto zako zitatimia upesi kuliko ukiwa peke yako au
ukiwa na watu wanaokurudisha nyuma.
NIFANYE BIASHARA NA NANI?
Biashara ina changamoto nyingi. Una bidhaa nzuri, lakini
wateja wanakataa kununua. Wafanyakazi pasua-kichwa wanakukosesha usingizi. Una
mipango mizuri lakini hauna rasilimali za kutosha kufanikisha malengo yako.
Ukiwa peke yako, changamoto hizi zinaweza kukutia wazimu.
Lakini ukiwa na mshirika mzuri, mambo yanaweza kuwa
tofauti. Kwa sababu hii, kila mmiliki wa biashara anahitaji angalau mtu mmoja
kwa ajili ya kubadilishana mawazo au kushirikiana kukuza biashara.
BIASHARA NI WATU, LAKINI SIYO WOTE WANAFAA
Haya ndiyo maswali ambayo yanawakosesha usingizi wamiliki
wa biashara.
1. Nifanye
biashara peke yangu au nitafute mshirika?
2. Nitajuaje
kama nafanya biashara na mtu sahihi?
3. Kuna
madhara yoyote kufanya biashara na ndugu?
4. Na
vipi kuhusu marafiki – wanafaa kuwa washirika wa biashara au hawafai?
Soma kitabu cha Mtu
Sahihi Wa Kufanya Naye Biashara na utapata majibu ya maswali haya yote na
mengine mengi.
HAKUNA SABABU YA KUTESEKA PEKE YAKO
Pengine na wewe unapitia mahangaiko haya:
·
Sijui jinsi ya kuchagua watu sahihi wa
kufanya nao biashara
·
Sijui kama nifanye biashara peke yangu au
nishirikiane na watu wengine
·
Naogopa watanifanyia fitina au kunisaliti
Soma Mtu Sahihi
Wa Kufanya Naye Biashara na
utagundua siri ya kutimiza malengo yako kwa kutumia rasilimali za watu wengine.
NIKISOMA KITABU HIKI NITAPATA NINI?
Utakaponunua Mtu Sahihi Wa Kufanya Naye Biashara…
1.
Utajua biashara yako inahitaji nini
2.
Utajifunza jinsi ya kupata rasilimali
unazohitaji
3.
Utagundua WATU WATANO ambao wanakurudisha nyuma
na kwanini unatakiwa kuwaepuka
4.
Fomla ya kuchagua watu ambao watakusaidia
kutatua changamoto zinazokukabili na kukuza biashara yako
5.
Ndani ya kitabu hiki kuna hekima safi ambayo
itakufundisha mikakati ya kukuza biashara yako kwa kujiamini
6.
Makosa ambayo watu wengi wanafanya
wanapoingia kwenye ushirika wa biashara
7.
Mbinu za kupata mtaji, ujuzi na rasilimali
nyingine unazohitaji ili kufanikisha malengo yako
8.
Kosa KUBWA ambalo pengine na wewe unafanya
unapoajiri wafanyakazi
9.
Siri za kutengeneza muundo wa biashara
10. Utaepuka
kupoteza pesa na muda kwa kushirikiana na watu ambao wanakurudisha nyuma
11. Na
kadhalika…
KUTANA NA MTU SAHIHI WA
KUKUSHAURI KUHUSU BIASHARA
Kama alivyofanya katika
vitabu vingine, Vianney Mahimbi ameandika vitu ambavyo amevipitia katika
maisha. Na kisha, ametoa mwongozo ambao unaweza kuutekeleza hatua-kwa-hatua.
Kabla ya kuandika kitabu
hiki, Vianney amewahi kufanya ushirika wa biashara na watu mbalimbali – kuanzia
ndugu, jamaa, marafiki na watu baki. Lakini pia, baada ya kufanya kazi ya
kuwashauri wamiliki wa biashara na wakurugenzi wa mashirika ya kijamii; Vianney
ameona na kushuhudia mengi.
Katika kitabu hiki, Vianney
anamshirikisha msomaji uzoefu wake katika namna iliyopangiliwa na kutekelezeka.
Baada ya kusoma kitabu hiki,
utaweza kusema kwa ujasiri, “Huyu Hapa! Mtu Sahihi Wa Kufanya Naye Biashara.”
KITABU HIKI KIMEANDIKWA KWA
AJILI YA NANI?
Kila mmiliki wa biashara
anahitaji kufanya biashara na watu sahihi. Lakini, kitabu hiki kitakufaa zaidi
kama…
·
Una wazo la biashara lakini hujui wapi pa
kuanzia
·
Unahitaji rasilimali muhimu kama vile pesa,
ujuzi, uzoefu na kadhalika
·
Unamiliki biashara na unataka mikakati ya
kukuza biashara yako
·
Unataka kujua kama mshirika wako wa biashara
anafaa au hafai
·
Hujui mtu sahihi wa kufanya naye biashara
Hata kama hauna mpango wa kushirikiana na watu wengine, kitabu hiki kitakupatia mikakati kabambe ya kukuza biashara yako.
Upo tayari kukutana na mtu
sahihi wa kufanya naye biashara? Kitabu hiki kimeandikwa kwa ajili yako.