Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Uzuri Wa Gereza Hazina Iliyo Sahaulika2 - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

Uzuri Wa Gereza Hazina Iliyo Sahaulika

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
2,500 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 08, 2025
Product Views:
113
In category:
Sample

Uzuri Wa Gereza Hazina Iliyo Sahaulika AUDIOBOOK

Muda wa simulizi ni dakika 35:00. Gerezani ni mahali ambako watu wenye tabia na hulka mbaya wasiostahiri kuishi katikati ya jamii wanalazimishwa kukaa kinyume na mapenzi yao bali kwa mujibu wa matakwa ya Kisheria, gerezani kwa ujumla wake ni mahali pabaya sana. Binafsi nilibahatika kuingia na kuishi kwa siku 110 ndani ya gerezani kuu la Butimba Mkoani Mwanza nchini Tanzania, nikituhumiwa kuuwa watu wawili na kumjeruhi vibaya mtu mmoja kwa kutumia silaha za moto (bunduki) na kijadi (panga, sime na mshale) kisha kupora shilingi za kitanzania millioni ishirini (Tsh 20,000,000.00). Nasema nilibahatika kwa sababu baada ya kupata fursa hiyo adhimu ya kuingia gerezani, nilijikita katika kufanya upelelezi wa kisiri ndani ya gereza hilo kwa muda wa siku 60 mfululizo, kitendo ambacho ni hatarishi kwani kinapingana na sheria za Jeshi la Magereza, matokeo ya upelelezi huo ndicho kilicho nisukuma kukuandalia haya masimulizi. Watu wengi sana leo ukiwemo na wewe unayesoma muhtasari huu sasa kwa kawaida huwa mnajiona kuwa mko huru uraiani nje ya gereza, taarifa rasmi kwako ni kwamba wengi wenu ni wafungwa ambao mmo gerezani mkitumikia adhabu za vifungo vya miezi, miaka, maisha na hata wengine mkisubiria kunyongwa hadi kufa pasipo kujua. Hebu chukua hatua binafsi kujifanyia tathimini je, katika maisha yako uko huru ama umo ndani ya kifungo cha gerezani kati ya magereza haya ninayo kutajia. Je? Moyo wako uko na uchungu ulio ibuliwa na Mahusiano, Uchumba, Ndoa na Maisha ya familia, kama jibu lako ni ndiyo Baba, Mama, Kaka au Dada umo gerezani! Je? Moyo wako uko na uchungu ulio ibuliwa na Huduma, Kazi, Biashara, na Taaluma, kama jibu lako ni ndiyo uwe ni Askofu, Shehe au mtu baki wewe ni mfungwa umo gerezani! Je? Moyo wako uko na uchungu ulio ibuliwa na Siasa, Uongozi na Utawala, kama jibu lako ni ndiyo Mheshimiwa umo gerezani! Je? Moyo wako uko na uchungu ulio ibuliwa na ugonjwa na Maradhi, Mazingira na Uchumi, kama jibu lako ni ndiyo jipe moyo kwani umo gerezani! Je? Moyo wako uko na uchungu ulio ibuliwa na Umaskini, kama jibu lako ni ndiyo ndugu yangu hilo nalo ni gereza! Hayo yote ni magereza kwa sababu yanamuondolea Mwanadamu uhuru wa kufanya atakavyo na kudhihirisha matokeo chanya kuhusiana na Maisha yake ya kila siku.Masimulizi ya kitabu hiki cha Uzuri wa Gereza Hazina Iliyo Sahaulika nimeyakusudia kimaalum kabisa kwa ajili ya kukuelimisha kuhusiana na elimu ya utandawazi wa maendeleo endelevu ya kiroho itakayo kupatia uwezo wa kujitawala kifikira na kuutawala ulimwengu wako binafsi unao kuzunguka. Usipange kutokusikiliza masimulizi ya kitabu hiki kwani ni ufunguo wa kufungulia mlango wa hilo gereza ulimofungwa pasipo kujua, ili uweze kuingia katika hatima njema ya maisha yako binafsi dhidi ya mazingira magumu yaliyo kukabili hivi sasa hapo ulipo na kujipambanua kuwa ni changamoto kwako.

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold