Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Vijue Viashiria Vya Magonjwa Ya Akili Katika Jamii Chanzo Athari Kinga Na Suluhisho Lake - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

VIJUE VIASHIRIA VYA MAGONJWA YA AKILI KATIKA JAMII: Chanzo, Athari, Kinga Na Suluhisho Lake

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 25, 2025
Product Views:
1,014
In category:
Sample

Jipatie nakala ya kitabu hiki \\\\\\\\\\\\\\\"Vijue viashiria vya magonjwa ya akili katika jamii:Chanzo, Athari, Kinga na Suluhisho lake.Pesa utakayoitumia kununua kitabu hiki hailingani na thamani ya maarifa utakayoyapata.KUMBUKA: “Ubora wa afya yako unategemea hali ya mwili, hisia zako, akili, masuala ya kiroho, mahusiano na watu wengine na mazingira yako.Mtu yeyote katika maisha yake anaweza kupata magonjwa ya akili.Mengi ya magonjwa haya hupona yenyewe ambapo mengine yanahitaji kutibiwa.Siyo rahisi kujua ni nani atapona bila kutibiwa.Mara nyingi kupona bila tiba inachukua muda mrefu na mgonjwa anaweza akaathirika sana kama akibaki katika hali ya ugonjwa kwa muda mrefu bila tiba\\\\\\\\\\\\\\\"

           Magonjwa ya akili ni kundi moja la magonjwa yasiyoambukiza ambayo yanazidi kuongezeka nduniani kote na hayana mwelekeo wa kupungua, huathiri afya ya mtu kuanzia jinsi anavyofikiri, anavyohisi, na anavyotenda..

            Taarifa za Shirika la afya duniani zinaonyesha kwamba nchi nyingi duniani hazilipi umuhimu unaostahili suala la afya ya akili katika jamii.Hali hiyo imesababisha huduma za maradhi ya akili katika nchi nyingi duniani kuwa duni na zisizothaminiwa.Matokeo yake ni wagonjwa wa akili pamoja na familia zao kunyanyasika, kutengwa na kudhalilishwa kimwili, kiakili na kihisia hii ni pamoja na watoto wenye matatizo ya akili utotoni.Tabia ya kunyanyapaa wagonjwa wa akili imejitokeza katika nchi nyingi kwa sababu yamejengeka mazoea ya kutothamini utu wao na haki zao za kibinadamu.

Ukisoma kitabu hiki hadi mwisho utajifunza yafuatayo:-

  1. Chanzo cha magonjwa ya akili katika jamii
  2. Jinsi jamii inavyoweza kuchangia/kusababisha magonjwa ya akili katika jamii husika
  3. Matatizo ya akili utotoni
  4. Makundi ya watoto waliohatarini kupata magonjwa ya akili
  5. Viashiria vya magonjwa ya akili utotoni
  6. Jinsi ya kutambua uwezo wa akili ya mwanao(Intelligence Quotient)
  7. Jinsi a kumtambua mtoto mwenye uwezo wa akili(IQ) chini ya wastani
  8. Viashiria vya magonjwa ya akili kwa vijana na watu wazima
  9. Magonjwa ya kimwili ambayo yanaweza kusababisha mtu kuugua ugonjwa wa akili yasipotibiwa kikamilifu
  10. Athari za magonjwa ya akili katika jamii
  11. Mbinu za kuimarisha uwezo wa akili yako na mahusiano bora katika jamii
  12. Jinsi ya kuishi na mtoto, mwenzi au ndugu mwenye afya mbaya ya akili
  13. Makundi ya watu waliohatarini kuwa walevi, wavuta tumbaku, bangi na madawa ya kulevya
  14. Nyakati ambazo huwafanya watu wengi kujiingiza kwenye dimbwi la ulevi, uvutaji tumbaku, bangi shisha na madawa ya kulevya
  15. Magonjwa ya akili ambayo muda wowote katika kipindi chochote cha maisha ya mtu anaweza kuugua
  16. Athari za pombe kimwili, kiakili, kijamii na kiroho
  17. Madhara ya pombe wakati wa ujauzito
  18. Athari za tumbaku maishani
  19. Kwanini tumbaku ina madhara makubwa zaidi kiafya ukilinganisha na pombe?
  20. Madhara ya tumbaku kwa watoto na vijana
  21. Madhara ya tumbaku kwa wanaovutishwa moshi wa tumbaku(second hand smoker)
  22. Madhara ya tumbaku wakati wa ujauzito
  23. Athari za tumbaku dhidi ya viungo mbalimbali mwilini
  24. Athari za kafeini mwilini
  25. Athari za kafeini wakati wa ujauzito
  26. Njia rahisi za kuvunja uraibu wa pombe, tumbaku, kafeini na madawa mengine ya kulevya
  27. Dalili za mfadhaiko
  28. Jinsi ya kushughulika na mfadhaiko maishani


Kitabu hiki kinayo mengi ya kujifunza yatakayo badili maisha yako na ya jamii inayokuzunguka

Je unahitaji kutimiza ndoto zako ukiwa na afya njema.? Mifereji ya mafanikio yako imo akilini mwako.Ukiharibu akili yako kwa namna yoyote umeharibu ndoto zako na ukiharibu ndoto zako umeharibu ndoto za kizazi chako.JALI AFYA YAKO YA AKILI.

Kupata hardcopy ya kitabu hiki lipia TSh 15,000/= Kisha tuma SMS/Piga 0686279021 ya muamala wako wa Malipo Jina Lubango Lucas Chikanda kitakufikia huko uliko kwa uaminifu mkubwa.

Nauri ya kusafirisha kitabu hiki kwa hapa Tanzania ni juu yangu.Mungu akubariki




     

More Products On Discount
More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
150,000 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold