Your Basket

Checkout | Shopping Cart
binadamu bado ni mnyama yule yule kama wengine anaye jitofautisha kimakosa na mazingira || GetValue

BINADAMU BADO NI MNYAMA YULE YULE KAMA WENGINE ANAYE JITOFAUTISHA KIMAKOSA NA MAZINGIRA

BINADAMU BADO NI MNYAMA YULE YULE KAMA WENGINE ANAYE JITOFAUTISHA KIMAKOSA NA MAZINGIRA

Binadamu amekuwa na mihangaiko mingi kwenye dunia ya kuhisi anaweza kufanya kitu zaidi kutumia mawazo yake kuisaidia ulimwengu kutenda kazi zake kwa anavyohisi anauwezo wa kufanya. Ni kweli binadamu anatambua nafasi yake kwenye mazingira ni ipi au anajipa nguvu inayoleta uharibu kwenye mazingira kwa jina la kuboresha mazingira. 


Ni kweli binadamu anauwezo wa kutambua upungufu wa ulimwengu na akautatua au hata yeye mwenyewe bado haja jitambua ni nani katika mazingira yake. Kama tukiishi kwa kujitofautisha na mazingira basi tutataka kuyaendesha kwa jinsi hisia na mawazo yetu yanavyo tuendesha kwa maarifa yetu madogo yenye uharibifu na tamaa ya ubinafsi. 


Matakwa ya binadamu ya kijamii na kibinafsi yamemfanya ajione yuko tofauti na viumbe wengine. Ila msingi mkubwa wa ulimwengu kwa viumbe matakwa huwa ni chakula na kuzaliana. Hata binadamu kwa kujiona na utofauti lazima aishi kwenye matakwa hayo makuu kwa utajiri na maarifa yote aliyo nayo anakuwa anatimiza mataka hayo ya ulimwengu kwa kujua au kutojua. Na hayo matwakwa humuweka sawa na viumbe wengine wote. 


Kwa vyovyote jamii ilivyo badili maisha ya binadamu jinsi ya atavyoweza kutimiza matwaka ya ulimwengu kwa kutumia fedha zaidi kuweza kupata mahitaji ya kula na kuendeleza kuzaliana, tumeweza kuongeza na matakwa yetu ya kiufahari yanayotupa wakati mgumu kuyatimiza na kuona maisha yamekuwa magumu zaidi kwetu kwakuwa tunahitaji vitu vingi zaidi ya vya msingi ulimwengu ulivyo tupangia kuhitaji kuishi.


Matakwa yetu ya kijamii na binafsi yametufanya tujione tuko tofauti na hatuendani na mazingira vilivyopo na kuishia kuharibu kila kitu kwa ajili ya kujinufaisha sisi wenyewe bila kujua nini kitatukuta kwa uharibifu huo. Tunahisi hakuna chenye thamani zaidi ya sisi kutimiza tamaa zetu. Tunakuwa tayari kuharibu chochote kwa furaha bila kujua huzuni tunayoiacha kwa matokeo yatayokuja kwetu wenyewe.


Ulimwengu umetufanya kuwa kitu kimoja kwa kutupa matakwa akilini mwetu yanayo tuongoza na kutunganisha na pengine kwa bila sisi kujua. Kutojitambua kwetu kuna haribu mzunguko wa asili kwa kutojua sisi ni moja ya muunganiko huo tunao takiwa kuuheshimu na kujua nafasi yetu kama binadamu. Hatupo juu ya mamlaka ya kuweza kutendea chochote mazingira kwakuwa hatujui chochote kuyakuhusu wala kujihusu sisi wenyewe zaidi tutaharibu kila kitu kwa jina la kuboresha na tutapata shida wenyewe.


Nb: Pengine tunahisi hapa si mahala petu kwa kuishi tunapita tu na kutojali mazingira yetu. Ila ukweli ujanja wetu wote unaletwa na haya mazingira yote tunayo yaona haya thamani kwetu.

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...