Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali
Best Seller

KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

0
1
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Aug 31, 2020
Product Views:
24,325
In category:
Sample

DIBAJI Nimepata wasaa wa kusoma vitabu vingi sana katika maeneo ya maendeleo binafsi na ukuaji wa kifikra hata hivyo nikiri kwamba nilipokishika kitabu hiki nikasema wawooo! Nimejikuta nakisoma tena na tena, sio ili nipate cha kukisemea bali nimejikuta ninavutiwa na kuguswa mno na mpangilio, muundo na maarifa ya kina ambayo mwandishi ameyawasilisha. Mwandishi, ameingia katika orodha ya waandishi wachache na adhimu sana katika lugha ya Kiswahili, wanaoandika aina hii ya maarifa. Jambo kubwa la kujivunia katika kitabu hiki ni kwamba mwandishi amefanya utafiti wa kina na kuwasilisha maarifa kwa namna yake. Naweza kusema hiki ni kitabu kilichojipambanua mno kwa maana kwamba hakikufanyiwa tafsiri ya waliyoandika wengine bali kimeleta mawazo halisi na uvumbuzi wa mwandishi. Kongole kwa mwandishi! Ni hakika kwamba muda huwa haubadilishi chochote, bali unachokifanya ndani ya muda ndicho huamua mabadiliko utakayoyapata. Mwandishi katika kitabu hiki ameeleza kwa namna ya kipekee namna bora ya kutumia muda. Katika maisha kuna namna mbili za kufanikiwa. Ya kwanza ni kujifunza kwa kukosea na ya pili ni kujifunza kutoka kwa waliotangulia. Njia ya kwanza ni ndefu mno, maana utalazimika kugundua kila kitu wewe mwenyewe na itakuchukua muda mrefu. Njia ya pili ni fupi na itakuchukua muda mfupi sana kufanikiwa. Hata katika Biblia, mathalani, Mungu anasisitiza kwamba ni vema kuchukua muda na kuyatazama maisha ya waliotangulia ili kujipatia raha nafsini mwetu, yaani furaha na mafanikio ya maisha. Mwandishi katika kitabu hiki ameturahisishia mno, maana pamoja na uvumbuzi wake mwingi pia anatuletea hekima zilizounganishwa kutoka kwa rundo la waliofanikiwa katika maeneo mbalimbali. Mimi nimeandika vitabu takribani 11 hadi sasa katika maeneo ya uchumi na familia. Kwa uzoefu wangu katika uandishi wa vitabu ninakiri kwamba kitabu hiki kina upekee mkubwa sana tena wa namna yake. Ndio maana kitabu hiki nathubutu kukiita kuwa ni hekima nyingi ndani ya kapu moja. Utakapokisoma mwanzo hadi mwisho utathibitisha hilo. Mwandishi amefanya kazi nzuri mno kushughulika na vile mtu unavyoweza kuboresha hatma yako. Wale ambao huwa wanadhani mafanikio ni jambo la bahati nasibu, mwandishi anawanoa huo uvimbe wa fikra kwa msumeno wa maarifa ndani ya kitabu hiki. Ndio maana nimependa sana alipoeleza habari ya kujiingiza katika orodha. Ohoo, kumbe mafanikio sio bahati nasibu bali ni suala la kuamua, kutendea kazi uliyoyaamua na kupata matokeo. Suala la kupata mafanikio ni uamuzi wako binafsi na mwandishi anasema hujachelewa kabisa! Hiki ni kitabu ambacho ninapendekeza kisomwe kuanzia kwa vijana wadogo mpaka wazee. Kwa namna kitabu hiki kilivyo, kina hekima kwa rika zote. Kwa kuwa kina maarifa yenye chembechembe za kutengeneza na kuibua vizazi ni kitabu ambacho kinafaa kusomwa na watu wa elimu zote. Ingalikua amri yangu ningesema kitabu hiki kisomwe na kila mwanafunzi wa chuo kikuu, kisomwe na kila mfanyabiashara na mjasiriamali, kisomwe na kila mfanyakazi na kisomwe na kila mtu mahali popote alipo maadam anajua kusoma. Kuna mambo ndani ya kitabu hiki ambayo yakiingia na kupokelewa katika mioyo ya watu mahangaiko yatapungua sana kwa taifa na kwa mtu mmoja mmoja. Hongera kwa kushika nakala ya kitabu hiki, naamini muda utakaoutumia kukisoma pamoja na fedha uliyotumia kukinunua ni uwekezaji wa thamani sana na utakaokulipa vizuri sana maishani mwako na katika vizazi vyako vingi vijavyo Albert Nyaluke Sanga(SmartMind) Mwandishi & Mjasirimali Mwandishi wa vitabu kama: Gia Kubwa, Umeiweka wapi Talanta yako? na Barua Ya Siri kwa wanandoa miongoni mwa vingi alivyoandika hadi sasa.

WATU WANASEMAJE KUHUSU KITABU HIKI?

 

MIMI NAMFAHAMU GODIUS

Ninamfahamu Godius si tu kwa kupitia maandishi yake bali kwa kupitia maisha yake. Jinsi anavyoishi ni darasa tosha la mtu yeyote mwenye nia ya kufanikiwa.

Nilipoanza kusoma kitabu hiki sikukoma kuacha kwani kimegusa maisha yangu na baadhi ya mambo niliyoyapata humo nimeanza kuyafanyia kazi na nimeanza kuona maajabu makubwa.

Unataka kuwa mbunifu? Soma kitabu hiki. Unataka kuwa kinara kwenye kipaji chako? soma kitabu hiki?

Unataka kuwa kiongozi kwenye maisha yako? Soma kitabu hiki.Unataka maisha yenye furaha na ya kuacha alama? Majibu yote yanapatikana humu kwenye Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni.

Imani yangu ni kwamba unaweza kuanzia hapo ulipo na kufika popote ili mradi akili yako umeipa ruhusa. Kila mtu amezaliwa mshindi, hakuna aliyekuja duniani kuwasindikiza wengine. Wewe ni wa tofauti, kuwa wewe, acha kujilinganisha na wengine, kujilinganisha kunabagua.

Asante sana Godius Rweyongeza kwa kitabu hiki kinachotafakarishi, kinachotia hamasa na kinachotupa dira ya kuishi maisha kwa utimilifu.

Edius Katamugora Mtunzi Yusufu Nina Ndoto

 

 

 

MWANDISHI KATUMIA LUGHA NYEPESI KUONGEA MAMBO MAKUBWA YA KIMAFANIKIO

Kila binadamu ndani kabisa ya moyo wake ana tamanio kubwa la kufanikiwa, yaani ikutoka ngazi ya chini kwenda ngazi ya juu katika Nyanja mbalimbali za Maisha. Kwa lugha nyepesi “Kutoka sifuri mpaka kileleni.

Lakini changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni njia sahihi za kupita au kanuni za kufuata ili kufikia hatima hiyo.

Mwandishi Godius Rweyongeza amejaribu, kwa kadri ya uwezo wake, kutumia lugha nyepesi na mifano halisi ya kumsaidia mtu kuweza kufuatana kutimiza azma ya mafanikio. Amezungumza kiundani jinsi ambavyo binadamu anaweza kutumia uwezo wa utashi aliopewa na Mwenyenzi Mungu katika kujiletea maendeleo binafsi katika Nyanja zote za Maisha.

Ni matumaini yangu kuwau naposoma kitabu hiki utaweka katika matendo yale yote utakayojifunza ili uweze kupata matokeo bora yatakayokuwa chachu chanya kwa wengine pia.

Nakutakia usomaji mwema na utekelezajiwa yale yote utakayojifunza.

 

Anthony Luvanda

Mjasiriamali na Mhamasishaji.

 

KAMA HUJUI NAMNA YA KUWEKA MALENGO, MWANDISHI AMEKUSAIDIA KUFANYA HIVYO KWENYE KITABU HIKI.

“Usipowaambia watu kuhusu mafanikio yako bila shaka hakuna atakayekuja kuyajua” Donald Trump

 

Acha Mimi nikuambie mafanikio yangu ili uyajue kupitia kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Ukitaka kujua mafanikio yako anza kusoma kitabu hiki cha kutoka sifuri hadi kileleni. Kwani utagundua uwezo mkubwa wa kufanikiwa ulioko ndani yako, kwanini unajichelewesha kupata ushindi ambao uko ndani yako?

 

Kama hujui kabisa namna ya kuweka malengo hatua kwa hatua ili yaweze kukusaidia kutoka sifuri hadi kileleni, basi mwandishi na mtaalamu wa kilimo cha bustani (Horticulture) Godius amekusaidia kufanya kazi hiyo kwenye kitabu chake cha kutoka sifuri hadi kileleni.

 

Ukiona mtu amefanikiwa kutoka sifuri hadi kileleni jua kuna siri kubwa nyuma ya ushindi.

 

Ninapendekeza kila anayetaka kufanikiwa, na hajawahi kusoma kitabu chochote kile basi kitabu hiki ni cha lazima kusoma kwa mtu makini anayeanzia chini kabisa na kutaka kufikia kileleni. Ni kitabu kinachokuonesha  mchakato wa mafanikio kutoka sifuri hadi kileleni.

 

Kila la heri rafiki yangu katika usomaji wa kitabu hiki.

Mwl. Deogratius Kessy

Mwalimu, Mwandishi na Mjasiriamali.

http://kessydeo.home.blog

 

 

HIKI NI KITABU CHA KARNE YA 21

Kujitoa bila kujibakisha, kusimamia jambo bila ya kurudi nyuma,  pamoja na kugundua uwezo wa ajabu aliouweka Mungu ndani yako, hivi vitakusaidia kufika hapo unapotaka kufika.

 

Kitabu hiki kimeanza kwa kwanza kwa kumsukuma mwandishi ujiuliza kwa nini wengine wamefika walipokusudiwa na wengine hawafiki, majibu yake yakiwa ndani ya kitabu hiki, yanagusa kuhamasisha na kufundisha, hiki ni kitabu cha karne ya 21,hivyo kila mmoja anapaswa kukisoma.

 

Mwalimu Adebert Chenche

Mwenyekiti wa taasisi ya VIPAWA LINK ASSOCIATION

 

 

 

 

NI KITABU CHENYE MAARIFA MENGI SANA.

 

Ni kitabu chenye maarifa mengi sana. Kwa uhakika atakayekisoma na kuyafanyia kazi ataweza kupiga hatua kubwa katika kutimiza malengo yake

NTANGEKI NSHALA

 

 

 

More Products On Discount
7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

More Products From This Seller
Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

GetValue Recommendations
5,000 Tsh.

Sold by: Denis Mpagaze

10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

10,000 Tsh.
(0.8)

Sold by: PJ PROJECTS

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold