
MAISHA NI FURSA:ZITUMIE ZIKUBEBE
Maisha ni Fursa: Zitumie Zikubebe
\r\n U | \r\n
shawahi kuona hili? Mtu\r\nanaambiwa kuwa kuna fursa fulani, anakimbilia kuifanyia kazi. Kabla hajatulia anasikia\r\nkuwa kuna fursa nyingine ambayo nayo anaikimbilia. Hivyo, anajikuta kuwa yeye\r\nkila mara ni mtu wa kudaka fursa hii, kisha kuachana nayo na kudaka fursa\r\nnyingine.
Wakati huohuo kuna watu\r\nwagumu kuziona fursa. Ndio maana mtu anaweza kuwa katika eneo fulani, ila haoni\r\nfursa zilizopo. Akatokea mgeni kutoka mbali na kuona fursa kwenye eneo hilo,\r\nkisha huyo mgeni akaanza kuifanyia kazi hiyo fursa. Ndio unakuta na mwenyeji\r\nanakimbia ili na mwenyewe aanzishe kitu hichohicho ambacho ameona mgeni\r\nanafanya. Muda mwingine unaweza kukuta mpaka watu wanaoneana gere mpaka\r\nwanafanya fujo ili uachane na hicho kitu unachofanya. Ubora wa fursa ni kuwa\r\nzipo nyingi tu ila wachache sana ndio ambao huwa wanazitumia huku wengine\r\nwakiendelea kulalamika kuwa hakuna fursa.
\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n\r\n
Kwenye kitabu hiki unaenda kujifunza\r\nkila kitu unachohitaji kujua kuhusu FURSA na namna ambavyo unaweza kuzitumia\r\nfursa. Je, upo tayari?