MAKOSA 12 YANAYOKUNYIMA WATEJA INSTAGRAM
EBook hii itakusaidia Kuanza kupata WATEJA WA KUTOSHA kutoka Instagram kuja kwenye BIASHARA YAKO - baada ya kufanya Marekebisho kwenye Makosa 12 Yanayokunyima wateja wengi sasa hivi
Je umekuwa ukitumia Nguvu kubwa sana kutangaza bidhaa zako (au huduma) kwenye mtandao wa Instagram kwa Njia za kawaida na za kusponsor matangazo... lakini HAUPATI WATEJA WA KUTOSHA wa kukusaidia kuwa na Mauzo makubwa na Kuongeza Faida kwenye biashara Yako?
Hii eBook (PDF) imeandikwa kwa ajili Yako.
Sio PDF kama zingine ulizosoma zilizokuwa na mambo ambayo watu wameyakopi na kupesti kutoka YouTube na Google.
Yaliyomo ndani ya hii PDF ni mambo niliyoyafanyia kazi kwa zaidi ya Miaka 3 kwa kukosea na kupatia (kwangu binafsi na kwa wateja niliyokuwa nawahudumia).
Mwisho wa siku, nikagundua makosa 12 yaliyokuwa yananifanya nisipate wateja Instagram.
Nilipoyafanyia kazi, nilianza kupata wateja wengi zaidi (Instagram), Mauzo yangu ya kila mwezi yakaanza kupanda na Faida ikaanza kuonekana.
Yote hayo nimeamua kukuandikia na wewe kwa lugha rahisi ya KISWAHILI ndani ya hii PDF ili usiishie kukata tamaa kwa kudhani Instagram Haina wateja.
Mtandao wa Instagram una wateja unaowahitaji, ila haya makosa 12 ndio yanayokurudisha nyuma (kwa kujua au kutokujua)