Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ukombozi Wa Fikra - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali
Best Seller

UKOMBOZI WA FIKRA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
5,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Nov 24, 2020
Product Views:
13,222
In category:
Sample

Mara baada ya kupata Uhuru wa Bendera, Mwl. Julius Nyerere alielekeza nguvu katika Uhuru wa Fikra maana aliamini bila Ukombozi wa Fikra, watanzania wataendelea kuishi utumwani. Kwahiyo akapeleka vijana wengi karibu kila kona ya dunia kuutafuta Ukombozi wa Fikra kupitia elimu. Lakini kwa bahati mbaya wengi wakaenda kupambana na mitihani badala ya ujinga. Wakarudi na fikra hatarishi kwa rasilimali za nchi. Mpaka mwalimu anaondoka duniani watanzania bado tunamwayamwaya katika Uhuru wa Bendera. Mwalimu katuachia uhuru ambao mwenye nacho ndio binadamu na asiyenacho ni takataka. Uhuru wa wachache kuishi kama malaika na wengi kuishi kama mashetani. Uhuru unaowagawa watu kwa kipato na elimu. Uhuru wa bendera ni sawa na kuvaa suruali isiyo na zipu harusini. Uhuru wa bendera umetujengea nidhamu ya woga kwa manufaa ya wachache kutunyonya kutokana na uoga wetu. Tunahitaji uhuru kamili. Ule uhuru unaoanzia kichwani, yaani uhuru wa fikra. Uhuru utakaotusaidia kuyaona mambo katika uhalisia wake. Kichwani pakiwa vizuri hatutapoteza muda kukimbizana na samaki bwawani kama tunataka kuwakamata. Badala yake ni kuwakaushia maji yote tu. Kumbuka “Fikra zinazoongoza akili yako ni muhimu zaidi ya kiasi cha akili ulizo nazo,” alisema David J. Schwartz kupitia kitabu chake cha, “The Magic of Thinking Big.” Fikra sahihi zinahitaji utulivu wa akili. Kuwa na muda wa kufikiri ndilo chimbuko la maendeleo yote duniani. Tunahitaji kuwa na karakana za kufikiri akilini. Badala ya kufikiri umaskini tulionao ni mapenzi ya Mungu, tufikiri umaskini kama matokeo ya kutofikiri vizuri. Mungu ametupa rasilimali nyingi ambazo kama zingelitumika kwa faida yetu, zingeliweza kutuinua tukawa matajiri. Tufikiri kwanza ndipo tutende. Kwame Nkrumah alisema, “Matendo pasipo mawazo ni upofu, mawazo pasipo vitendo ni utupu.” Kumbe saa ya ukombozi wa fikra ni sasa. Tusitegemee kama kuna mtu atakuja kutukomboa isipokuwa ni sisi wenyewe aliimba Bob Marley katika kibao cha, “Redemption.” Bila fikra huru tutaendelea kushuhudia watawala wakishindana katika matanuzi. Akinunua BMW, mwenzake ananunua Benz. Hii ndio itikadi ya Bongo. Kumbuka, “Leo upo pale ambapo mawazo yako yamekuleta, kesho utakuwa pale ambapo mawazo yako yatakupeleka. Mtu anavyofikiria katika akili yake anakuwa hivyo, na anavyochagua anakuwa hivyo.” Kumbe tuna kila sababu ya kuchagua kufikiri vizuri ili kuwa na taifa lenye maendeleo. Hivyo basi jiongezee maarifa kwa kusoma kitabu hiki na hakika utakombolewa kifikra. Mfalme Sulemani alisema, “Akili ya mtu mwelevu hutafuta maarifa na sikio la mtu mwenye busara hutafuta kusikia maarifa.”

Denis Mpagaze ni mwandishi mashuhuri wa makala za viongozi na msuala ya  kijamii kama vile ndoa, elimu, maisha, biashara, mapenzi, tamaduni, imani na dini. Makala nyingi za Mpagaze husimuliwa na Ananias Edgar kupitia mitandao ya kijamii na redio mbalimbali. Kabla ya kujikita katika uandishi, Mpagaze alikuwa mwalimu wa chuo kikuu cha Mt. Agostino cha Tanzania yaani SAUT kwa zaidi ya miaka 12 lakini aliamua kuachana na ajira na kufanya shughuli za kuitumikia jamii ya kiafrika. Andika DENIS MPAGAZE katika Youtube na utaona kazi zake nyingi! 

More Products On Discount
7,000 Tsh. 2,999 Tsh.

Sold by: Said Maumba

Best Sellers List
Best Seller
10,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

GetValue Recommendations
10,000 Tsh.
(1)

Sold by: PJ PROJECTS

12,000 Tsh.

Sold by: Germano Mbelwa

5,000 Tsh.

Sold by: Sabas Patrick

10,000 Tsh.
(0.8)

Sold by: PJ PROJECTS

25,000 Tsh.

Sold by: PJ PROJECTS

Old is Gold