SIRI 7 ZA MAFANIKIO YA KIROHO NA KIUCHUMI
Biblia inasema katika kitabu cha Isaya 45:3 “...Nami nitakupa hazina za gizani na mali zilizofichwa na za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israel”. Kwa hiyo, ninachoamini ni kwamba, baada ya kumaliza kusoma kitabu hiki maisha yako yatabadilika asilimia mia moja katika anga za biashara, ndoa, huduma ya Mungu, masomo kama roho yako ifanikiwavyo, Amina!!!.
Ndugu msomaji, awali ya yote ningependa nimshukuru Roho Mtakatifu kwa kunifunulia siri hizi saba za mafanikio ya kiroho na kiuchumi. Ni ufunuo wa pekee kwa neema ya Mungu, ambao kupitia kitabu hiki utakwenda kupokea siri hizi. Katika kitabu cha Waefeso 3:5, Maandiko yanasema, “Siri hiyo hawakujulishwa wanadamu katika vizazi vingine, kama mitume wake watakatifu na manabii zamani hizi katika Roho Mtakatifu”. Ndugu msomaji wangu popote ulipo duniani namwomba Mungu kupitia Roho Mtakatifu akupe macho ya rohoni ili uweze kuona na kuelewa siri zilizofichika katika kitabu hiki. “SIRI SABA ZA MAFANIKIO YA KIROHO NA KIUCHUMI.” Kama vile mtume Paulo anavyomwomba Mungu wa mbinguni awape waefeso macho ya rohoni katika kumjua Mungu (Efeso 1:17-18), nami namwomba Mungu akupe macho ya rohoni na ufahamu wa hali ya juu katika kusoma na kuelewa siri hizi za ajabu zitakazokuwezesha kufanikiwa kiroho na kiuchumi.