
HABARI NJEMA IMEKUFIKIA
“Kitabu hiki “Habari Njema Imekufikia” ni barua ya upendo kutoka kwa Mungu Baba kwa kila moyo unaotafuta tumaini na uzima wa kweli. Kwa lugha nyepesi na yenye nguvu ya kiroho, Dkt. George Macha anatufikisha kwenye kiini cha Injili ambacho ni Upendo wa Mungu unaookoa, unaoponya, na unaoweka huru. Hii ni zawadi halisi ya kiroho kwa kizazi chetu. Ni muhimu isomwe, ichukuliwe kwa uzito, na ipokelewe kwa upendo na moyo wa unyenyekevu.”
NAKUPENDA- ni neno linalo ogopwa kutumiwa na watu wengi hata wengine kutumia pasipo kujua maana yake halisi hadi kupelekea watu wengi kuumizwa na kutojua maana halisi ya Upendo. Ninamshukuru Mungu Baba kwa ajili ya kitabu hiki kizuri ambacho kimezidi kunionesha juu ya Upendo mkuu wa Mungu Baba kwetu ambao ndio wa kweli na mkuu kuliko wote. Ninaamini kwa kuzidi kuuelewa Upendo huu wa Mungu Baba juu yetu basi wengi tutaponywa na kuufanya ‘Mwili wa Kristo’ kuwa sehemu salama zaidi duniani. HAKIKA MUNGU BABA ANANIPENDA SANA!