DHAMBI ASILI YA MAUTI KWA MWANADAMU
Dhambi ndio kiini cha matatizo yote leo duniani, lakini inashangaza mwanadamu haogopi dhambi amabacho ndicho chanzo cha mauti yote duniani. Kitabu hiki nimoja ya taifi zilizofanywa na mwandishi wa kitabu, kuna ukweli mkuu kuwa kifo kinaogopeka na mwanadamu yoyote Yule awe masikini awe jairi wote wanaogopa kifo tukifiwa tunasikitika kuondokewa na wapendwa wetu na ndugu zetu lakini je dhambi zinazo tuzunguka tumeshawahi kujiuliza kama ndio chanzo cha yote Magonjwa yote unayoweza kuyaona duniani asili yake ni dhambi, Nihali ya mwanadamu kutokumsikiliza mungu fikiria dhambi ya uzinifu halafu angalia jinsi gani imeleta HIV inavyosumbua watu duniani kote. Kitabu hiki kinaangalia (souce) au sababu inayosababisha kifo wengi wanaangalia kifo badala yakuangalia nini chanzo, ukijuwa chanzo cha kitu chochote kile kinacho kusumbua unakuwa na asilimia nyingi za kulishinda jambo linalokukabiri, Nikweli kifo sio habari nzuri wanaondoka wapendwa wetu familia zinabakia na watoto yatima wengine wanakosa hata kusoma vizuri, Yanaibuka mahangaiko mengi lakini nini chanzo (what is the souce of death?) yani nini chanzo cha kifo? Je ni ugonjwa? Je ni ajari? Kama ni hayo nayenyewe yana sababishwa na nini bado utakuta ni dhambi ukikosa utiifu wa sheria ni dhambi maana sheria za dunia zinatokana na sheria za mungu (Yehova) ukiachia mbali zile zenye utashi wa kibinadamu kama usiasa n.k.
Tunatakiwa kuwa watu wa kutubu muda wote Wanadamu dhambi inatuharibia mahusiano yetu na Mungu. Tunatakiwa kuepuke dhambi kwa kila njia ila peke yako huwezi unatakiwa kufanya nini soma kitabu hiki upate maarifa yakutosha.