TAIFA LA ISRAELI LILIVYOFUTWA KWENYE RAMANI YA DUNIA
Kikubwa kilichomo katika kitabu hiki ni uchambuzi wa kina wa Vita kuu tatu kati ya Wayahudi na himaya ya Roma iliyopelekea taifa la Israeli kutokuwepo kwenye ramani ya dunia kwa muda wa miaka 1813 tangu mwaka 135 BK hadi mwaka 1948 lilipoundwa tena.
TAIFA LA ISRAELI LILIVYOFUTWA KWENYE RAMANI YA DUNIA
Wana wa Israeli baada ya kuishi Misri kwa muda wa miaka 430 hatimaye mwaka 1447KK walianza safari ya miaka 40 jangwani wakiongozwa na nabii Musa kwenda Kanaani, mwaka 1406KK baada ya kifo cha Musa, waliongozwa na Yoshua wakaanza kumiliki nchi ya Kanaani.
Baada ya kuingia katika nchi ya ahadi walikaa humo muda wa miaka 1541 tangu mwaka 1406KK hadi 135BK waliposhindwa vita kuu ya tatu kati yao na Warumi ambapo waliangamizwa wengi na wengine kuuzwa kama watumwa wakatawanyika duniani kote.
Jina la kitabu ni TAIFA LA ISRAELI LILIVYOFUTWA KWENYE RAMANI YA DUNIA katika kitabu hiki zimemulikwa vyema vita kuu tatu kati ya Wayahudi na Warumi na mauaji ya kimbari yaliyopelekea Wayahudi kuikimbia nchi yao.
Kwa muda wa miaka 1803 tangu tarehe 04, August, 135BK walikuwa nje ya nchi yao, hadi tarehe 14, Mei, 1948 kwa jinsi ya ajabu taifa lao lilipoundwa tena sawa na manabii walivyotabiri. Karibu tujifunze.