Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Amri 67 Za Uandishi Bora - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

AMRI 67 ZA UANDISHI BORA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
12,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jun 10, 2025
Product Views:
176
In category:
Sample

Licha ya kasi kubwa ya fani ya uandishi na uboreshaji wa ubunifu wa shughuli za uandishi, uandishi wa karne ya 21 unakabiliwa na makosa mengi ya kiufundi/kiutaalamu. Ustadi wa juu wakati mwingine hauzingatiwi na weledi wa uandishi umepwaya sana kutokana na ongezeko la makosa katika machapisho yanayohusu dhamira za kijamii, kisiasa, kiuchumi na kitaaluma.\\r\\nWewe unafikiri ni nini ambacho kina poromosha soko la wasomaji dunia ya leo? Makosa ya kiufundi ndiyo yanayochangia kuporomoka kwa soko la wasomaji. Ubora wa kazi za uandishi ni kikwazo kikubwa sana kwa wasomaji ikiwa waandishi hawatashughulikia mapema. Mtu anapokuwa anasoma kazi zako anaweza kufurahishwa au kukerwa na umakini au makosa yako uliyoyafanya kipindi cha uandaaji wa chapisho lako. Nguli wa kufuata amri za uandishi, kazi zao hutamba kwa vizazi vingi sana kutokana na umahiri wao katika kuzingatia amri za uandishi ambazo wasomaji wa vitabu wanazipenda. \\r\\nNimewahi kusikia wasomaji wakitoa kauli hizi ambazo sio nzuri, ‘’Waandishi wengine ni waganga njaa tu ‘’. Waandishi wengine hawana jipya kazi kutafsiri vitabu vya wazungu’’, ‘’Waandishi wengine ni wavamizi wa fani za wengine’’. Kauli hizi ndugu yangu zinauma sana lazima ujiandae kuzikwepa kwa kila kitabu chako. Ujue maana ya hizo kauli ni sawa na kusema kwamba ‘’kazi uliyoandika ni dhaifu mno na haina jipya lolote na pesa nilizotumia kununua kitabu chako nilipoteza tu!\\r\\nHapa inamaanisha kwamba, kama wasomaji wako wangejua vizuri kilichomo ndani ya kitabu chako basi wasingenunua hicho kitabu chako. Ni sawa na kusema kwamba badala ya kununua chapisho lako, afadhali hizo pesa zingefanya manunuzi ya kitu kingine. \\r\\nSiku moja nilikuwa nasoma kitabu cha mwandishi maarufu Afrika Mashariki nikiwa safarini kutoka Tanga kwenda Dodoma (04/10/2021 saa tatu na dakika 31) abiria mmoja niliyekuwa nimekaa nae alivutiwa na kitabu nilchokuwa ninakisoma. Baada ya muda kidogo, aliniomba kile kitabu asome kidogo ili baadae aende kukinunua pia. Baada ya kukisoma kwa dakika tano akabaini makosa zaidi ya matatu kisha akabadili sura na kunirudishia akisema ‘’kuna tatizo kwenye kitabu chako naona kina makosa sana na siwezi kukisoma’’. Nilikipokea kile kitabu akanionesha makosa hayo. Safari yangu ilibadilika na kuwa nzito kwani niliwaza hii changamoto ya vitabu vyenye kuudhi wasomaji itaisha lini? Ungekuwa wewe ungewaza kitu gani? Siku hiyo niligundua kwamba wasomaji wa vitabu wa kizazi kipya hawako tayari kusoma vitabu vyenye makosa na vyenye hoja dhaifu.

AMRI HIZI 67 SIO ZA MAJARIBIO ZITUMIE ZIKUSHANGAZE

More Products On Discount
Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

GetValue Recommendations
Old is Gold