
MABADILIKO YA HOMONI NA JINSI YA KUYAKABILI
Mabadiliko ya homoni na jinsi ya kuyakabili
Mwili wa binadamu ni mashine ya kipekee inayofanya kazi kwa usahihi mkubwa chini ya usimamizi wa mfumo wa homoni. Homoni ni kemikali ndogo zinazozalishwa na tezi mbalimbali mwilini na kusafirishwa kupitia damu kwenda kwenye viungo na tishu tofauti. Hizi ndizo zinazosimamia karibu kila kitu katika maisha yetu ya kila siku: kuamka na kulala, jinsi tunavyohisi, njaa, uzito, nguvu za mwili, hamu ya tendo la ndoa, uwezo wa kupata watoto, na hata jinsi tunavyokabiliana na msongo wa mawazo.
Lakini pamoja na umuhimu wake, homoni hubadilika kulingana na umri, jinsia, mtindo wa maisha, na hali ya kiafya. Wakati mwingine mabadiliko haya hutokea kwa utaratibu wa kawaida mfano wakati wa kubalehe, ujauzito au uzee lakini mara nyingine yanaweza kuathiri afya na maisha yetu kwa njia zisizotarajiwa. Mwanamke anaweza kupata mzunguko wa hedhi usio wa kawaida, mwanaume akakosa nguvu za kiume, au mtu yeyote akapitia mabadiliko ya uzito na hisia bila kujua chanzo ni nini.
Kitabu hiki kimeandikwa ili kutoa mwanga juu ya mabadiliko ya homoni na jinsi ya kuyakabili kwa njia salama na zenye ufanisi.Utajifunza:
Homoni kuu zaidi ya 17 zinazohusiana na mwili wa mwanadamu na kazi zake, athari zake zikipanda au zikishuka.
Mabadiliko yanayotokea katika hatua mbalimbali za maisha (balehe, ujauzito, baada ya kujifungua, ukomo wa hedhi kwa wanawake (menopause) na ukomo wa uzazi kwa wanaume (andropause)).
Athari za homoni kwenye afya ya akili, ngozi, nywele, na uzito.
Vitu vinavyoweza kuharibu usawa wa homoni bila wewe kujua.
Njia bora za kudhibiti mabadiliko haya kupitia chakula, mazoezi, mtindo wa maisha, tiba asilia na msaada wa kitaalamu.
Lengo ni kuhakikisha kila msomaji anapata maarifa ya kujitunza, kufahamu mwili wake, na kuchukua hatua mapema kabla matatizo hayajawa makubwa.
Kwa hiyo, safari hii ya maarifa ni mwaliko kwako kujua zaidi kuhusu mwili wako na kuishi maisha yenye afya, nguvu na furaha licha ya changamoto za mabadiliko ya homoni.
Kitabu hiki ni mwongozo wa afya ya kila siku, kwa wanawake na wanaume, vijana na wazee, ili waweze kuelewa kinachoendelea kwenye miili yao na kuchukua hatua sahihi za kujilinda.
Usikose nakala ya kitabu hiki ujifunze maajabu ya miili yetu kupitia homoni
Kupata hardcopy ya kitabu hiki ni TSh 12,000/= Kisha tuma SMS/Piga 0686279021 ya muamala wako wa Malipo Jina Lubango Lucas Chikanda kitakufikia huko uliko kwa uaminifu mkubwa.Nauri ya kusafirisha kitabu hiki kwa hapa Tanzania ni juu yangu.Mungu akubariki
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godfrey Ngaleya
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher