JINSI YA KUGUNDUA KIPAJI CHAKO NA KUKIFANYA KIKUINGIZIE KIPATO:Siri Ya Mafanikio Yako
Jifunze njia rahisi za kugundua kipaji chako na jinsi unavyoweka kukifanya kikuingizie kipato
Jinsi ya Kugundua Kipaji Chako na Kukifanya Kikuingizie Kipato: Siri ya Mafanikio Yako ni mwongozo wa kipekee unaokufundisha namna ya kutambua zawadi na uwezo wa kipekee uliopewa na Mungu, kisha kuutumia ili ufanikiwe kimaisha.
Kitabu hiki kinakufungua macho kuona kwamba kila mtu ana kitu cha thamani ndani yake, na kwamba kipaji hakipaswi kubaki kimefichwa. Kinaeleza hatua kwa hatua:
- Jinsi ya kugundua kipaji chako
- Namna ya kukikuza na kukiendeleza
- Mbinu za kukibadilisha kipaji kuwa fursa ya kipato
- Shuhuda za watu waliotumia vipaji vyao kufanikisha maisha yao
- Siri za kujenga nidhamu, bidii na ubunifu ili kufanikisha ndoto zako
Kitabu hiki si cha kusoma tu bali ni cha kutenda.Ni darasa la maisha litakalokufanya uache kuishi kwa mazoea na kuanza kutumia kile ulicho nacho kuijenga ndoto yako.Kama umewahi kujiuliza“Ninaweza nini hasa?” au “Nitafanikisha vipi maisha yangu?” basi majibu yako yapo humu ndani.
Hii ndiyo siri ya mafanikio yako kipaji chako ni tiketi yako ya kufikia ndoto kubwa zaidi maishani.
Hii ni kazi ambayo imefanikishwa na mwandishi mwenye vipaji tofauti LUBANGO L CHIKANDA, chini ya usimamizi wa Chikanda Medical Publisher ambayo imedhamiria kuielimisha jamii katika nyanja mbalimbali za maisha.
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher