
MBINU ZA KUJIKINGA NA SARATANI MBALIMBALI
Kitabu hiki kipo kukusaidia kujifunza\r\n\r\nMaana ya saratani na aina zake\r\nKwanini watoto wanapata saratani na utazijuaje zake kwa mtoto\r\nSaratani huanzaje na hueneaje\r\nVitu vinavyochangia uwepo wa magonjwa ya saratani\r\nDalili za awali za magonjwa ya saratani\r\nNi vipimo gani hutumika kuchunguza iwapo una saratani\r\nNjia zinazopendekezwa kupunguza uwezekano wa kupata saratani\r\nNa mengine mengi kuhusu saratani na mtindo wa maisha
Saratani ni miongoni mwa magonjwa yanayozidi kuongezeka \r\nna kusababisha vifo vya watu wengi duniani. Ugonjwa huu \r\nhutokea wakati sehemu ya mwili inapokua na kuongezeka bila \r\nutaratibu na kusababisha uvimbe. Kwa kawaida saratani huanza \r\ntaratibu na kuchukua muda kuonyesha dalili zozote.Pia dalili za awali \r\nhaziambatani na maumivu hivyo kusababisha wagonjwa wengi \r\nkuchelewa kutafuta matibabu. Mara nyingi saratani haina maumivu \r\nmwanzoni na ni ngumu kugundua hasa kama iko kwa ndani. \r\nUtafiti umeonyesha kuwa karibu nusu ya saratani zote zingezuilika \r\nkwa njia ya mabadiliko katika mtindo wa maisha.Saratani ni moja ya \r\nmatatizo makubwa duniani leo, ambapo asilimia 12.5 ya vifo vyote \r\nduniani husababishwa na saratani (2007).Kiwango hiki kinaweza \r\nkuongezeka kutokana na mtindo wa maisha ulioshamiri miongoni \r\nmwa wanaume na wanawake leo. Kidunia saratani inaua watu wengi \r\nzaidi kuliko wote wanaokufa kwa VVU/UKIMWI, Kifua kikuu, na \r\nMalaria vikiungana pamoja(Mtindo wa Maisha uk14; Afya \r\nMaridhawa uk 6). \r\nKila mwaka zaidi ya watu milioni 12 hugunduliwa kuwa na saratani \r\nulimwenguni (Mtindo wa maisha uk14). Saratani inaonekana kuwa \r\nugonjwa mpya wa mlipuko katika nchi zinazoendelea ambapo taasisi \r\nza nchi hizo zinazohusika na mapambano ya ugonjwa wa saratani \r\nzinaonekana hazijajiandaa vya kutosha kukabiliana na ongezeko la \r\nv \r\nMbinu za kujikinga na saratani mbalimbali: Lubango L. Chikanda \r\nsaratani. Lakini ni vizuri kujua ya kuwa kwa kila saratani tano \r\nzinazotokea mbili zinaweza kuzuilika na pia ingawaje saratani hazina \r\ntiba, nyingi zinaweza kuondolewa kabisa na zisirudi tena. \r\nKwa sababu ya ongezeko la magonjwa yatokanayo na mtindo wa \r\nmaisha yaliyoenea duniani kote kitabu hiki kitakusaidia wewe, \r\nfamilia yako, na jamii inayokuzunguka kwa ujumla mbinu za \r\nkujikinga na magonjwa ya saratani.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza