
JINSI MILANGO YAKO YA FAHAMU INAVYOWEZA KUJENGA AU KUBOMOA TABIA YAKO
Jinsi Milango Yako Ya Fahamu Inavyoweza Kujenga Au Kubomoa Tabia Yako
Kila Mtu anayesoma kitabu hiki ana milango ya fahamu inayofanya kazi kila siku, hata kama hajawahi kuifikiria kwa undani. Milango hii ni njia ambazo akili na moyo wako hupokea taarifa, mawazo, hisia na matukio kutoka ulimwengu wa nje. Hii ndiyo sehemu ambayo huamua tabia yako, imani yako,na hata hatima yako.
Ukiifananisha maisha yako na nyumba, basi milango ya fahamu ni kama milango na madirisha ya nyumba hiyo. Unachoruhusu kuingia ndicho kitakachoamua harufu, usafi, na hali ya ndani ya nyumba. Vile vile, kile unachoruhusu kuingia katika akili yako kitaamua hali ya maisha yako ya ndani hisia, mawazo, na matendo yako.
Watu wengi hawajui kwamba nguvu kubwa ya kuunda au kubomoa maisha yao ipo kwenye yale wanayoruhusu kupitia macho yao, masikio yao,pua yao, kinywa chao, na hata hisia zao. Mara nyingi mtu husema, “Hii ni kitu kidogo tu, haitanidhuru,” bila kujua kuwa kile kidogo kinarudiwa kila siku na hatimaye kinakuwa tabia ya kudumu.
Biblia inatuonya katika Methali 4:23: “Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.” Moyo unaotajwa hapa si tu wa mwili, bali akili yako ya ndani sehemu ya fahamu. Ndipo milango ya fahamu inapokaa.
Kwa hivyo, kuelewa na kutunza milango hii si jambo la hiari, bali ni wajibu.Ukichunga milango yako, utalinda tabia yako. Ukiacha milango yako wazi bila ulinzi, adui atapata nafasi ya kupanda mbegu mbaya ambazo zitavunja maadili yako, amani yako na hata ndoto zako
Kitabu hiki kipo kukusaidia katika safari yako ya kuelewa kila lango la fahamu, jinsi linavyofanya kazi, hatari zake, na namna ya kulilinda ili maisha yako yajengeke kwa heshima na baraka.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godius Rweyongeza
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher
Sold by: Chikanda Medical Publisher