MBINU 10 ZA MAFANIKIO SIRI ZA KUFANIKIWA KIUNGU
Mafanikio ni kitu cha muhimu sana ,na ni cha lazima kwa kila mwenye uhai, na kila anaeishi katika dunia hii, yaani mwanadamu.Mafanikio si ombi, bali ni kitu cha lazima, na ndiyo maana kila mtu hupanga kufanikiwa, hakuna mtu anaepanga kufeli, utakuta mtu anatumia kila mbinu ,ili aweze tu kufanikiwa, na ndiyo maana katika dunia hii kitu ambacho kinahitaji mapambano ni Mafanikio pekee yake. Watu wana enda kwa waganga wa kienyeji , wanapewa masharti magumu na wanayatekeleza , lengo ni kwamba maisha yawe mazuri. Wengine wanaua wenzao lengo ni kufanikiwa. Watu wanafanya biashara ,lengo ni kufanikiwa , na Mungu ametuleta duniani ili tufanikiwe , tuishi katika maisha ya Mafanikio. Ukisoma kitabu cha Mhubiri 3:12. \\\\\\\\\\\\\\\"Najua ya kuwa kwaa binadamu liko jambo moja la kufaa kufurahi na kujifurahisha muda wote aishipo. 13 Sote inatupasa kula na kunywa na kufurahia Matunda ya kazi zetu .Hayo ni Majariwa ya Mungu.\\\\\\\\\\\\\\\"Unaona mwandishi anaelezea hakuna jema kupita kwao kufurahi na kufurahia mema ya kazi zao, yaani Mungu mwenyewe anataka tufanikiwe. Na Mafanikio Asili yake ni rohoni , na ndiyo maana ni muhimu sana kutafuta nguvu za Kiroho , ili uweze kufanikiwa . Soma nami hapa. 3 Yohana1:2 Mpenzi naomba ufanikiwe, katika mambo yako yote, nakuwa na afya yako,kama vile roho yako ifanikiwavyo. Na mafanikio yamegawanyika katika sehemu mbili, -mafanikio yanayo anza na mtu binafsi. -mafanikio yanayo anza na familiya. Niukweli usiyo pingika, kila mtu anahitaji mafanikio ,kwa maana Mafanikio ni mfumo wa Mungu ,aliouweka kwa mwanadamu ili Mwanadamu aweze kuuishi. Na ndiyo maana mtu aliye umbwa na Mungu,huambatana na maisha, na maisha huambatana na mafanikio, na Mafanikio ni mpango wa Mungu ili kila mtu afanikiwe. Ni maombi yangu kwa Mungu kila mtu aweze kufanikiwa katika kila jambo na kila maneno ,na kila anacho kufanya kilicho chema akafanikiwa katika jina la Yesu Kristo, Amen.
Mafanikio ni Utoshelevu , na ni utele wa kila ,kinachohitajika na kisichohitajika, pia Mafanikio ni baraka toka kwa Mungu. Na ndiyo maana Mungu alipo muumba mtu alimbarikia akawaambia zaeni mkaongezeke, Hapa kuzaa siyo tu kuzaa watoto wa kibinadamu tu, hata chochote kinacho tokana na Mawazo ni kitu kilichozaliwa . Kumbuka kuwa chochote tunachokiwaza ni matokeo ya mbegu iliyopandwa ndani ya Fahamu zetu, inaweza ikawa mbegu inayo tokana na Mungu au mbegu inayotokana na shetani. Lakini hapa si zungumzii mbegu , ila tunazungumzia kuwa Mafanikio ni Baraka . Tusome hapo waefeso. Waefeso 1:3 \\\" Atukuzwe Mungu Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo , aliyetubariki kwa baraka za ROHONI, katika Ulimwengu wa roho ndani yake Yesu Kristo.\\\". Mafanikio ni utajiri wa kila kitu, utajiri wa Afya, Mafanikio ni utajiri wa Amani, ni utajiri wa Mali, mifugo na fedha , na watu walio sahihi , na wanaosimama pamoja nawe kuhakikisha unafanikiwa kutimiza maono uliyonayo.
2 Mambo ya nyakati 9:22 \\\" Basi Sulemani aliwapita wafalme wote kwa Mali na Hekima\\\". Mafanikio ni nguvu ya Mungu, ndani ya mtu, ambayo iko ndani ya Ulimwengu wa Kristo Yesu, lakini wengi hawaelewi kuwa Mafanikio ni Baraka za Mungu, na ni nguvu za Mungu. Ambazo Mungu mwenyewe alidhihifadhi kwaajili ya kila mtu anae kuja duniani. Watu wengi kwa kuto elewa kwao, kuwa Mafanikio ni Baraka za Mungu, wamejikuta wakijiumiza sana, na kuwaza sana, wakizani mafanikio ni kujiumiza kwa kufanya kazi ngumu, hili suala si la kweli kabisa. Ndugu yangu mpendwa, kufanikiwa sijambo gumu, kama unavyodhani,Mafanikio ni kitu rahisi sana, ila ugumu wa kufanikiwa uko, kwenye kanuni,maana Mafanikio yana kanuni, na ili mtu aweze kufanikiwa lazima afuate kanuni, bila kufuata kanuni ni ngumu kufanikiwa,.