
NYAMBOGE: Safari Ya Majuto, Tumaini Na Ushindi
Katika kijiji kidogo cha Sombanyasoko, kijiji chenye historia ya milima ya Somba na Nyasoko na watu wake wa kabila la Wakurya na Wajaruo, alizaliwa binti mrembo ajulikanae kwa jina Nyamboge. Alikuwa kipenzi cha familia, kipaji cha darasa na kioo cha jamii. Uzuri wake uliovutia macho ya kila mtu ulimletea heshima – lakini pia ulimfungulia milango ya majaribu makubwa.\r\nSafari yake ya maisha inasomeka kama simulizi ya kusisimua na ya majonzi: kutoka mwanafunzi mwenye ndoto kubwa, hadi msichana aliyejikuta akining’inia kwenye mitego ya marafiki wabaya na tamaa za dunia. Hatimaye, anajikuta akisafiri kwenye njia yenye giza – njia ya umalaya na majeraha yasiyofutika.\r\nLakini ndani ya dhoruba hii, kuna mwanga wa matumaini. Baada ya kugundua kuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI, Nyamboge hachukui hatua za kukata tamaa. Badala yake, anasimama tena, akapambana, akafanikisha masomo yake, na hatimaye akapata maisha mapya yenye heshima, upendo na familia.\r\nKitabu hiki si hadithi tu – ni kioo cha jamii ya Kitanzania. Kinazungumzia changamoto halisi za vijana, nguvu ya maamuzi tunayoifanya kila siku, na uzito wa marafiki tunaowachagua. Kila sura inaishia na funzo maalum kwa vijana, likitoa mwongozo wa kupita katika changamoto za maisha bila kupoteza heshima wala matumaini.
Hadithi hii ya “Nyamboge: Nuru ya Matumaini Maishani” ni zao la fikra, uzoefu, na miale ya matumaini ambayo huchanua hata katikati ya giza. Ni sehemu ya mfululizo wa BADILI TABIA MAISHANI: Hadithi Asilia za Kiafrika, mradi unaolenga kuwagusa vijana na jamii kwa ujumla kupitia simulizi zinazojikita katika maisha halisi ya Kiafrika. Nyamboge si jina la kubuni. Ni sauti ya wengi waliopitia giza la maisha, waliodondoka, lakini hawakufa moyo. Kupitia hadithi hii, msomaji atashuhudia maumivu, mapambano, na hatimaye ushindi wa kweli unaojengwa juu ya kujitambua, maarifa, na kusamehe. Lengo kuu si kuwahukumu wahusika, bali kuwapa jamii yetu nafasi ya kutafakari, kujifunza, na kuanza upya. Kwa kuwa kukata tamaa maishani ni dhambi kubwa, hadithi hii ni wito wa matumaini mapya.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godfrey Ngaleya