NUKUU ZA MAISHA
Hapo Ulipo Kuna Wapo waliokuwa Hapo Na Wakashinda: USIOGOPE
Kukosa mtaji imekuwa ni sababu kuu ambayo wengi wanapenda kuitumia unapowauliza ni kwa nini hadi sasa hawajaanza biashara? Ukweli ni kuwa wengi sio kwamba wamekosa mtaji huo wanaosema bali wamekosa mtaji wa aina ya mawazo. Wewe binafsi kama unasema huna mtaji basi hujui ni kitu gani unachotaka kufanya. Ukweli ni kwamba hakuna kitu kisichokuwa na mwanzo mdogo kama utakifahamu vizuri. Kuna namna bora ya kuanza na kile ulichonacho na ukafikia kile unachotaka kuwa nacho. Kusema kwamba huna mtaji ni kufunika yale mambo ya kweli ambayo yanasababisha wewe usianze kuchukua hatua. Unakuwa unafunika woga wako, uvivu, na kutotaka mabadiliko.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza