TAMBUA UWILI WAKO NDANI YA UMOJA WAKO AKILINI MWAKO NA UJISHANGAE MWENYEWE
Kinacho ongelewa hapa ukitaka ukielewe usiangalie maneno elewa kinachongelewa kwa kujihusisha nacho moja kwa moja. Maneno yana njia nyingi za kuelezea kitu moja. Usijiweke kwenye kizuizi cha maneno yanavyo fafanua jambo na utashindwa kuwa na uwanja mpana wa kuelewa ukiji akisia mwenyewe.
Usichanganyikiwe kwa kusikia uwili wa akilini mwako, hivi ndivyo jinsi ilivyo. Akili zetu zina uwili ndani ya umoja wake. Na ina tupa shida sana kwenye maisha yetu kwa kutolielewa hili. Kuna akili ya ufahamu na akili ya kumbukumbu katika utendaji wa mfumo wetu wa ubongo. Na si lazima iwe majina yaliyo tumika bali ni kuweza kuelewa tu kinacho ongelewa kwa urahisi.
Embu tuelewe zaidi katika ufafanuzi ufuatao
Akili ya ufahamu ni ipi?
Ni upande wa akili ambao una husika na ufahamu wa kinacho endelea nnje na ndani yetu na wajibu wa kuamua kiutendaji. Hii ni akili ya jinsi unavyo pokea taarifa kwa milango yako ya fahamu katika kila wakati uliopo na kuweza kuamua na kuchagua kwa kutaka utendaje katika mapokea hayo. Na kikubwa akili ya ufahamu ina weza kupokea taarifa kama mawazo katika akili ya kumbukumbu kwa uzoefu wako jinsi ulivyo tenda zamani. Ni kama umepata ajili na hukumbuki hata kitu kimoja pale ni unakuwa na akili ya ufahamu tu bila kuwa na mawazo mengine yoyote ya kukumbuka.
Akili ya kumbukumbu na ishara ni ipi?
Ni upande wa akili ulio umbwa ujitegemea kiutendaji. Ni vyote ambavyo umesha vihifadhi katika akili yako na kuvitambua kwa kutaka na vingine nnje ya matakwa yako na kuingia kwenye mfumo wako wa kiakili na kuwa tabia. Utambulisho wako wote wa jinsi ulivyo hua unatokea hapa.
Kwa ufupi ni akili iliyo shikilia jinsi ulivyoishi na watu, wanavyokujua matendo yako unavyopenda na usivyo penda, unacho ogopa na ujasiri wako na mengi mengi yanayo jumuisha uhusika wako kwa jinsi ulivyoishi. Akili hii ya kumbukumbu huwa msingi wake inajiendesha yenye "automatic", utavyo pokea taarifa na utavyotenda ina jihifadhi kwa jinsi ulivyojiwekea kuona hicho kitu.
Na mfumo wa akili ya kumbukumbu msingi wake ni kama mzani wa kukuweka sawa na kukutaarifu kwa mawazo jinsi ulivyoishi kipi kinaweza kuwa hatari na salama kwenye wakati uliopo. Imani zetu, tabia zetu, mbegu ya mawazo yetu, asilimia kubwa ya maisha yetu yanatokea katika mfumo huu na ni duara linalotupa utambulisho wetu wa jinsi tulivyo.
Madhara tunayopata kwa kutotambua uwili wetu wa akili
Kila akili ipo huru inajitegemea ndio maana ni rahisi kuona kama kuna ushindani ndani ya akili yako mwenyewe. Ukiona kumbukumbu zinataka kushindana na wakati uliopo au wakati uliopo unataka kushinda tabia zinazo wakilisha kumbukumbu basi ujue huna ubayana ndani ya akili yako.
Mawazo yetu ni msingi wa akili ya kumbukumbu kuwasiliana na akili ya ufahamu katika wakati uliopo. Na mawazo yetu kimsingi hayapo ndani ya matakwa yetu, utachopenda na usichopenda vyote utavipokea kwa milango yako ya fahamu na vitahifadhiwa sawa na vitakuja kwenye mawazo muda wowote vinapotoka kutoka na mahitaji ya wakati huo.
Kwa kutoelewa hili tumejitengenezea uadui mkubwa katika kuishi kwetu ndani yetu. Tutasingizia shetani kanipitia na kuona kama unashindana na mtu mwingine ndani yako si kweli bali ni wewe kutokuwa na ufahamu na uwili wa akili yako na kupambana na mawazo yako mwenyewe. Maisha ya furaha yetu yote yanamalizwa na mapambano ndani ya akili yetu wenyewe kwa kutotambua ni sisi wenyewe tuna jipambanisha. Mawazo yetu wenyewe yamekuwa sumu yakutuangamiza.
Athari kubwa tunayoipata ni kujitafsiri kuwa sisi ni kumbukumbu zetu jinsi tulivyoambiwa na kushepiwa na mazingira yetu (udini, nchi, kabila au kujitafsiri kwa unachofanya) na kuona kama tuna waza vibaya na tusivyopenda tuwaze, inapelekea kuanza kujichukia wenyewe bila kujua mfumo wetu wa mawazo unafanya kazi kwa kujitegemea wenyewe.
Kupingana kwako kwa kutokuwa na mawazo hasi ni jambo lisilo wezekana, labda mazingira yako yote yawe chanya (kinachoingia ndio kinachotoka) na kutaka kudhibiti mawazo ndio chanzo cha kuleta vita isiyo na mwisho akilini mwako.
Na akili asili yake imejiweka kutafuta usalama na faraja, mawazo yetu huwa na msingi wa kutafuta usalama katika mazingira na na jinsi ya kuwa kwenye faraja. (Ukitaka kufanya kitu kisichokuwa ndani ya usalama wako lazima utanza kuwa na woga) na kama utaelewa lazima ujiulize kwanini naogopa nikifanya kitu nnje ya uzoefu wangu.
Kitu gani kina hitajika uweze kupata uelewa utao kufungua
Na huu ndio ukomavu "mature" wa mtu wenye maana. Kuwa huru kutoka kwenye kifungo cha mawazo na kujifahamu undani na thamani yako. Maana matitizo yote yanayo tuangamiza na kutupa shida tunayatengeneza wenyewe kwa kutojitambua tu. Tumejiwekea umuhimu kuishi ndani ya mifumo inayotufanya tujisahau kujitazama umoja wetu na ulimwengu.
Tukiacha upotofu wa kujitambua kwa dini zetu, nchi, utendaji kazi na hata jina si wewe ni halisi, tukiweza kuviweka pembeni na kuanza kujitafakari bila mawazo yoyote ndio mwanzo wa kupata mwangaza wa uhalisia wako na kujifahamu uhalisia wako mwenyewe.
Kwanza, tuweze kujua ina tulazimu sisi wenyewe kuweza kuona umuhimu wa kuweza kuweka vitu vyote pembeni na kuanza kujifahamu sisi wenyewe bila msaada wa maarifa ya mtu mwingine yeyote. Ukweli huu kuu elewa ni lazima ujione mwenyewe ndani yako ndio utaweza kupata mabadiliko ya kweli.
Lengo kubwa ni akili yako ya ufahamu na kumbukumbu (wakati uliopita na uliopo) kuweza kuwa kitu kimoja na kufanya kazi kwa utaratibu mzuri kwa kila uhitaji wake unapo hitajika kwa kuwa umeshapata ufahamu na huna ujinga wakukutenganisha tena akilini mwako.
Nb: Kuishi katika ufahamu zaidi wa kitu halisi unacho kutana nacho na kukielewa kama kilivyo bila kutegemea mfumo wako wa kumbukumbu kukuwekea giza lolote lile litalokuzuia kuona uhalisia ndio kitu kinacho hitajika.