• Call us +255 717 568 861

Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Mema Magazine - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

Mema Magazine

Ratings

Price:
5,000 Tsh.
Vendor:
Num added to cart:
0
Added to shop:
Apr 29, 2021
In category:
Sample

Mema ni jarida la vijana lililosheheni michongo kibao kwa ajili ya vijana. Ndani utasoma stori za vijana mashuhuri kama Hadija Jabiri, mjasiriamali maarufu wa kilimo biashara, fursa za mitandao ya kijamii, mbinu za usaili n.k. Kila unaponunua jarida hili unasaidia kusambaza katika mfumo wa nakala ngumu kwa vijana waliopo shule za sekondari.

Mema Magazine ni jarida la vijana linaloangazia michongo na mishe kibao zinazohusu afya ya uzazi, michezo, ajira na ujasiriamali, sanaa na uraia na simulizi za watu maarufu na wanaofanya vyema katika jamii. Ndani ya toleo hili la kwanza #Tumesomeka tumefanya mahojiano na Hadija Jabiri, moja ya wajasiriamali wakubwa na maarufu katika kilimo biashara. Shughuli zake zimejikita Iringa na chapa yao ya bidhaa za mboga mboga inayofahamika kama Eat Fresh imekuwa ikiuzwa katika masoko ya ndani na nje ya Tanzania. Alifanikiwa vipi kufika hapo alipo? Unafahamu Hadija alipata ujauzito akiwa bado mwanafunzi na hakukata tamaa kufikia ndoto zake?


Cooogi pia ni kijana anayefanya vyema katika miondoko ya Chill pop. Ni miondoko yenye swagga za kibongo na kimamtoni. Licha ya kuwa bado hajateka soko la ndani, muziki wake umekuwa ukifanya vyema katika mitandao ya kidijitali kama vile Spotify, Audiomark, Youtube n.k. Akiwa na wafuasi zaidi ya 10,000 katika mtandao wa Instagram, inamsaidia kusukuma kazi zake na kuwafikia wapenzi wake. Ingawa ana umri mdogo, ndoto yake inasukumwa na imani ya vipaji vyake lukuki ikiwemo uchoraji. Unadhani siku hizi kutoboa katika muziki unahitaji redio na Tv zipige nyimbo zako? Ukisoma stori ya Cooogi kuna mengi ya kujifunza.


Jarida lina stori nyingi za kukujenga na kukupa michongo ikiwemo ujuzi hitajika katika karne hii ya 21. Unazitambua fursa zilizomo katika mitandao ya kijamii? Huna mtaji na unafikiria namna gani utaweza kujiajiri? Unatambua mambo muhimu ya kuzingatia kabla hujaenda katika usaili? Yote utayapta ndani ya Mema Magazine.


KUMBUKA: Kila unaponunua jarida hili unasaidia kuchangia fedha kwa ajili ya uchapishaji wa majarida ambayo yatasambazwa kwa wanafunzi waliopo shule za sekondari ili kuwapa taarifa na maarifa sahihi.

Other products from this category