Fichuka: Discover Yourself In God
Through discovering God, You discover yourself
\"Kama lilivyo Jina la Kitabu FICHUKA, limesadifu yaliyomo ndani kuhusu maisha. Kila Neno ndani ya Kitabu hiki ni munyu na limeshikiliwa na Msingi wa Neno la MUNGU.
Kitabu kimebeba mambo muhimu yakuwezeshayo kutambua kusudi la Mungu katika maisha yako katika maeneo yanayokuhusu, kutambua thamani ya kusudi hilo, na kwa Namna gani unaweza ukalifikia.
Kitabu hiki kinakuchomoa kutoka KULE ULIPOJIFICHA na MADINI yale Mungu aliweka ndani yako.
Kitabu kinagusa kila Eneo linalokuhusu Kijana hadi kufikia hatma yako na Namna ya kushinda Changamoto zinazokukabili ili uweze kuishi maisha Safi yanayompendeza Mungu\"
- UPENDO SENI, Dar es Salaam.
\"Kitabu cha FICHUKA kina Siri nyingi zinazofichua Hazina kubwa Ndani ya maisha ya Mtu. Kinakupa kujua kusudi lako na Nguvu ya Kuzaliwa. Haijalishi ulizaliwaje au katika yapi, ila kusudi la wewe kuwepo lina Nguvu zaidi.
Kinakupa kujua THAMANI ya maisha yako na jinsi ya kutunza thamani yako na kuiheshimu. Kitabu cha Fichuka ni Mgodi muhimu sana ambao kila mtu anatakiwa Kuuchimba ili kufichua kile kilichofichwa ndani yake na Mungu mwenyewe.\"
- VIOLETH BURA, Dar es Salaam.