BIASHARA NI MAAMUZI
Watu wengi wanapenda mafanikio na wanatamani kuwarn
wafanyabiashara wakubwa, wawe na uhuru wa kifedha, narn
kujulikana kwa mafanikio yao. Lakini, wachachern
wanatambua kuwa mafanikio siyo matokeo ya bahati, bali nirn
zao la maamuzi sahihi yanayofanyika kila siku. Kitabu hikirn
kimeandikwa kwa ajili ya watu wanaotaka kujifunza kufanyarn
maamuzi bora katika biashara, bila kutegemea bahati walarn
miujiza. Hebu fikiria hadithi hii. Kijana mmoja aitwaye Musa alikuwarn
anataka kufungua duka la kuuza vifaa vya simu. Alikuwarn
ameweka akiba yake ya miaka miwili, na hatimaye alifikiarn
hatua ya kuchagua eneo la kufungulia duka. Alikuwa narn
chaguo kati ya maeneo mawili. Moja lilikuwa katika soko linalojulikana kwa msongamanorn
wa watu, lakini kodi yake ilikuwa kubwa. Jengine lilikuwarn
pembezoni mwa mtaa, liliendana na uwezo wake wa kodi, lakini lilikuwa na watu wachache sana. Musa alitumia siku kadhaa kusikiliza marafiki, kuombarn
ushauri, na kufanya tafiti. Alikumbuka kusudi lake la mudarn
mrefu siyo tu kufungua duka, bali kulijenga kuwa biashararn
kubwa ya vifaa vya kielektroniki. Mwishowe, alifanya uamuzirn
mgumurn
kuchukua eneo la ghali, lakini lenye nafasi ya kukua haraka. Alihama mtaani kwake na kuishi kwa rafiki ili apunguzern
gharama. Mwaka mmoja baadaye, duka lake likawa maarufu, na sasarn
alikuwa anaagiza mzigo moja kwa moja kutoka nje ya nchi. Hadithi ya Musa si ya miujiza ni hadithi ya maamuzi yenyern
malengo. Kila aliyefanikiwa katika biashara, kuna siku alikaarn
chini na akafanya uamuzi wa kubadili maisha yake. Kitaburn
hiki kinakualika kufanya uamuzi huo leo. Kila sura katika kitabu hiki imeandikwa kwa uangalifu, ikiwarn
na maarifa ya vitendo, mifano halisi kutoka Tanzania, narn
misingi bora ya kufanya maamuzi katika mazingira halisi yarn
kibiashara. Hiki si kitabu cha kusoma tu ni kitabu charn
kutenda. Ni mwongozo wa kufungua akili yako, kuelewarn
hatari za maamuzi mabaya, na kuona nguvu iliyopo kwenyern
maamuzi sahihi. Karibu sana. Hatima ya biashara yako ipo mikononi mwarn
maamuzi unayofanya leo. Nathaniel Jacob Mahundirn
Mwandishi & Mshauri wa Biashara




