Your Basket

Checkout | Shopping Cart
jipatie vitabu vya mwl. patrick sanga vilivyozinduliwa desemba 2025 || GetValue

JIPATIE VITABU VYA MWL. PATRICK SANGA VILIVYOZINDULIWA DESEMBA 2025

JIPATIE VITABU VYA MWL. PATRICK SANGA VILIVYOZINDULIWA DESEMBA 2025

Shalom, Kipekee namshukuru sana Mungu ambaye amenitia mafuta kuwa mmoja wa waandishi wa vitabu na masomo mbalimbali ya kiroho. Mathayo 13:52 imeandikwa: “Akawaambia, Kwa sababu hiyo, kila mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”


Kufuatia neema ya Mungu na mafuta hayo ya uandishi, nilianza kuandika masomo ya kiroho mwaka 2003 nikiwa mkoani Mbeya. Aidha, ilipofika mwaka 2006 ndipo nilianza kuweka masomo hayo kwenye blogu yangu ya kwanza yenye anuani ya www.sanga.wordpress.com. Pia katika mwaka huo wa 2006, ndipo niliandika kitabu changu cha kwanza.


Tangu wakati huo niliendelea kuandika masomo ya kiroho, vitabu vingine, na hata sasa ninaendelea. Naam, sitaacha, kwa kuwa najua nimepewa na nimeagizwa na BWANA mwenyewe kuandika.


Katika mwaka huu wa 2025 nimefanikiwa kuandika vitabu viwili vifuatavyo: SAFARI YA KUMTAFUTA NA KUMPATA MWENZA WA MAISHA KATIKA MAPENZI YA MUNGU NAMNA MWANAMKE ANAVYOWEZA KUZITUMIA NAFASI ZAKE ZA KIROHO KUBADILISHA MAISHA NA NDOA YAKE Uzinduzi wa vitabu tajwa ulifanyika siku ya Jumapili tarehe 28/12/2025, mkoani Mwanza.


Karibu ununue vitabu hivi ndani ya website hii ya www.getvalue.co kwa search title husika ili ujipatie ufahamu na maarifa. Naam, kwa kufanya hivyo utakuwa umechangia kazi ya uandishi wa vitabu vingine ambavyo Patrick Sanga anaendelea kuviandika.


Licha ya uandishi wa vitabu, Patrick Sanga ni mwandishi wa masomo ya neno la Mungu na mengine mahususi kuhusu Roho Mtakatifu, vijana, wanawake, ndoa, na siku za mwisho, nk. Ikiwa utapenda kusoma masomo hayo, tafadhali tembelea blogu za www.sanga.wordpress.com na www.sanga.co.tz. Utukufu na heshima vina wewe Yesu, wastahili BWANA wangu.


“…Utaiinua misingi ya vizazi vingi…” (Isaya 58:12)

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...