Your Basket

Checkout | Shopping Cart
je unamjua mteja wako || GetValue Inc

JE UNAMJUA MTEJA WAKO?

JE UNAMJUA MTEJA WAKO?

Baada ya kumsikiliza kwa muda wa dakika 10 akinielezea juu ya Ubora wa Bidhaa yake itakayoleta mapinduzi Sokoni...


Nikaamua nimwulize kwanza SWALI ili nijue kama tupo pamoja. 


"Hivi mteja wako ni nani ?"


Akatulia kwa muda, huku akiwa anatazama chini, kisha akanijibu, "Hii Bidhaa ni kwa ajili ya kila mtu anayeihitaji."


"Kila mtu anayeihitaji !" Nikamwuliza kwa mshangao, nikiwa nimemkodolea macho.


"Ndiyo, kila mtu anayeihitaji"


"Okay, huyo mtu anayeihitaji yuko wapi ?" Nikaendelea kumwuliza. 


"Huyo mtu yupo hapa hapa Tanzania. We huoni hii Bidhaa ilivyo nzuri, hata pakeji yake ipo freshi!"


"Hilo halina shida kabisa, nakupa big up. Lakini swali langu Lipo pale pale, nahitaji kumjua mteja wako."


"Bhana eh! Usinikatishe tamaa. We naona una Wivu na maendeleo yangu. Ngoja niondoke, usiniharibie siku yangu." Akajibu kwa msisitizo na kuondoka, huku akiwa anasonya.


Aiseeh! Kazi Ipo. 


Nirudi na kwako Mjasiriamali mwenzangu, au mfanyabiashara...


Je, Mteja wa Bidhaa au Huduma uliyonayo ni nani hasa?


Au nawe Upo kwenye kundi la "Kila mtu ni Mteja wangu?"


Hilo ni Swali la msingi sana unalopaswa kuwa na Majibu yake kabla ya kuingia Sokoni.


Sokoni kuna Watu wengi sana. Hivyo, Unapaswa kujua Watu wako ni akina nani. 


Ukiisha kumjua mteja wako na Sifa zake, itakuwa rahisi kwako kujua mahali pa kumpata.


Uliishawahi kumsikia machinga wa "Oya oya, pata madela makali hapa kwa gharama nafuu kabisa. Hata kwenye baridi halina shida" kwenye mtaa uliyojawa na Wanaume...


Huyo ni mfano hai wa mtu asiyemjua mteja wake mkubwa, pamoja na Mahali anapopatikana.


Umenielewa mpaka hapo? 

Anza kufanyia kazi, utaona Mabadiliko makubwa sana. 


Je, BADO UNA SWALI LO LOTE LILE LINALOHUSIANA NA UTAFUTAJI WA MASOKO PAMOJA NA MAUZO ?


Karibu sana, Uulize.


Kama ni Suala Binafsi, karibu sana INBOX kwa nambari 0764793105 WhatsApp. 


Au kwa EMAIL Lacksontungaraza@gmail.com


Lakini pia Unaweza ukapata kitabu changu cha "Mbinu 16 za kuongeza Mauzo kwenye Biashara Yako" kitakacho kubusti kwenye suala zima la Mauzo. 


Kumbuka: "USIPOMJUA MTEJA WAKO, HUTAJUA ALIPO."


BY LACKSON TUNGARAZA. 

@lacksontungaraza. 

Muasisi wa @lamaxdesigns.

0764793105 WhatsApp 


.

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...