Your Basket

Checkout | Shopping Cart
jinsi ya kupata isbn za vitabu nchini tanzania kirahisi zaidi || GetValue

JINSI YA KUPATA ISBN ZA VITABU NCHINI TANZANIA KIRAHISI ZAIDI

JINSI YA KUPATA ISBN ZA VITABU NCHINI TANZANIA KIRAHISI ZAIDI


WATU WENGI WAMEKUWA WAKINIULIZA INBOX  

"JINSI YA KUPATA ISBN ZA VITABU"


NGOJA NIJIBU HAPA ILI KILA MTU ASAIDIKE.




Kwanza kabisa,

" ISBN ni nini?" Ahsante Kwa kuuliza.



ISBN ni kifupi cha INTERNATIONAL STANDARD BOOK NUMBER.



Hiyo ni namba ya utambulisho wa kipekee wa kitabu chako duniani.



Na utambulisho huo unakuwa na tarakimu 13 (hii ilianza tangu mwaka 2007, zamani zilikuwa tarakimu 10).


Kwa mfano,

 *978-969-9792-35-9* 



Sasa...


 

ZINGATIA YAFUATAYO;


1. Kila kitabu kinatakiwa kuwa na ISBN yake - usitumie ISBN moja Kwa kila kitabu.


2. Ukitoa toleo jipya la kitabu (new edition) unapaswa kuweka ISBN Nyingine - Kwa sababu Kuna vitu ulivyoongeza au kupunguza katika kitabu chako.


3. Kila fomati ya kitabu unapaswa kuwa na ISBN yake. eBook iwe na ISBN, hardcopy iwe na ISBN yake, audiobook iwe na ISBN yake. Usitumie ISBN moja Kwa hizo fomati zote.


4. ISBN sio ya kutunga kichwani (kujitengenezea mwenyewe). Unapaswa Kwenda maktaba kuu ya wilaya au mkoa au taifa Dar es salaam kupata ISBN yako, au kuiomba kwa Njia ya mtandao (online).


5. ISBN ni Kwa ajili ya utambulisho tu wa kitabu chako, sio kwa ajili ya ulinzi wa kisheria. Ukitaka ulinzi wa kisheria (HAKIMILIKI) nenda COSOTA.


6. Si lazima kisheria kila kitabu kuwa na ISBN.


7. ISBN ni lazima Ikiwa unataka kuuza kitabu chako kupitia wauzaji wakubwa wanaotambulika; wa mtaani (bookstores & publishers) na wa mtandaoni (kama vile Amazon, Apple books, n.k), au kama unataka kiwepo katika maktaba za vyuo vikuu na maktaba kuu ya taifa.


8. ISBN sio lazima kama kitabu chako utakuwa unakiuza mwenyewe.


9. ISBN huonyesha kitabu chako kimesajiliwa katika mfumo wa kimataifa wa vitabu (Global Book Industry) - Kutambuliwa Rasmi kimataifa.



 HATUA ZA KUPATA ISBN* 


1. Nenda maktaba kuu ya wilaya au mkoa au taifa (National Library of Tanzania) jijini Dar es salaam ukiwa na kitambulisho chako (ID) pamoja na Ada ya usajili elfu 30 (au Nyingine yoyote watakayokuambia).


2. Utawaambia unataka ISBN ngapi; utapewa hata 5 kwa hiyo hiyo ada ya usajili.


3. Uwe na taarifa zifuatazo; jina la kitabu, jina la mwandishi, tarehe ya uchapishaji, muundo wa kitabu (kama ni hardcover, paperback, audiobook au eBook), jina la mchapishaji (Kama unachapisha mwenyewe, yaani Self-Publisher, utatumia jina lako au jina la biashara yako ya uchapishaji).


4. Wape email yako wakutumie ISBN pamoja na barcode yake.



 USISAHAU: Ukishachapa kitabu chako, hakikisha unapeleka nakala kadhaa maktaba kuu ya taifa Kwa ajili ya kumbukumbu - ndivyo sheria inavyoelekeza.


.

MWISHO KABISA:

1. Karibu @lamaxdesigns TuKUANDIKIE KITABU CHAKO 

2. Karibu @lamaxdesigns upate huduma za Book cover design, Book typesetting (kupangiwa vizuri KURASA za kitabu chako), transcription (Kubadilisha mafundisho yako ya kwenye SAUTI kwenda kwenye maandishi), printing, n.k.

.

.

WhatsApp namba: +255764793105.

.

.

#lamaxdesigns #layoutdesign #books #ebooks #chatgpt #aivideo

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...