Your Basket

Checkout | Shopping Cart
nyakati za ukimya || GetValue Inc

NYAKATI ZA UKIMYA

NYAKATI ZA UKIMYA

Walipofika pembezoni mwa mto walimkuta mwanamke mmoja mzee akiwa amekaa akisubiri kuvushwa na watu maana peke yake asingeweza kuvuka...

Wakamchukia na kumbeba kwa pamoja, mwingine akambeba kwa upande huu na mwingine kwa upande mwingine mpaka wakamfikisha ng`ambo palipo na nchi kavu, wakamshusha na kumuacha pale, yule mwanamke akawashukuru Sana nao wakaenda zao...

Wakiwa njiani yule monki mmoja akaanza kulaumu kwamba mgongo wake unauma Sana kwa sababu ya kumbeba yule mwanamke...yule monki mwingine akawa kimya tu huku akiendelea kusonga mbele...

Walipotembea Kama kilomita tatu hivi, yule monki akaanza kulia maumivu tena na Mara hii mpaka akashindwa kuendelea mbele ikambidi akae chini, akawa analalamika mgongo unamuuma Sana,ndipo akamuuliza mwenzake "Vp wewe mgongo haukuumi"? Yule monki akamwambia maneno machache ambayo nataka ujifunze hapa akasema

"Mimi nilimtua yule mwanamke maili kadhaa zilizopita kwa hiyo mgongo hauwezi kuendelea kuniuma"

Ndipo nikagundua kuwa mambo yaliyopita yanaweza kuwa kikwazo kikubwa Sana katika maisha yako Kama hautaamua kuyasamehe na kuendelea na maisha yako..

Kuna watu sababu kubwa inayosababisha msisonge mbele Ni visasi mlivyovibeba kutokana na kufanyiwa Mambo mabaya na watu wengine....

Kuna watu kinachowanyima amani sio kukosa fedha, sio kukosa mchumba, sio kukosa marafiki Bali kuendelea kushikilia maumivu ya marafiki mliotengana nao....

Kuna watu hamtaki kujiweka huru kwa kuwasamehe wengine matokeo yake mnalemewa na mizigo mioyoni mwenu..

Anayekutakia mema kwenye maisha Ni lazima akufundishe umuhimu wa kusamehe na kuachilia mambo fulani yapite katika maisha yako....

Hauwezi kuwa Bora Kama utaendelea  kumiliki visasi vya zamani, hauwezi kuwa Bora Kama hautakuwa na moyo wa kusamehe.

Kusamehe Ni kujipa Uhuru wewe mwenyewe kiasi Cha kuwa na wepesi wa akili hata Kama utakutana na waliokufanyia makosa..

Mwisho kila mtu Ni mkosaji, Lakini sio siku zote utakuwa mkosaji, Nia kusamehe maana Kuna watu wanabadilika, tua mizigo uliyojiwekea mwenyewe...songa mbele...

Sehemu nilipo Ni weak networked area kwa hiyo naweza tuma sms asubuhi ikafika jioni hivyo usinungunike Sana, na unaweza ukanitumia sms leo ikaingia kesho,usinungunike pia

@yurisdutch
yurisdutch@gmail.com


@Yuris Dutch

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...