Your Basket

Checkout | Shopping Cart
sio lazima uandike kitabu kikubwa sana || GetValue Inc

SIO LAZIMA UANDIKE KITABU KIKUBWA SANA

SIO LAZIMA UANDIKE KITABU KIKUBWA SANA

CHUKUA HUU USHAURI KATIKA UANDISHI WA VITABU

Sio Lazima uandike kitabu kikubwa sana ndipo ujisikie umetoa kitabu.

Ukubwa wa Kitabu unategemeana na mambo kadhaa; kama vile...

I. Ukubwa wa Wazo 

II. Aina ya Kitabu 

III. Kiwango cha taarifa na maarifa juu ya kile unachokiandika 


Sasa, kama Kitabu unachotaka kuandika hakina ulazima wa kuwa kikubwa sana, matharani #Page 100 kwenda mbele... USILAZIMISHE.

KITABU chako kinaweza kuwa na #Page chache, lakini kikabadilisha maisha ya watu wengi sana na kupendwa zaidi ya vitabu vingine vilivyo vikubwa._

Kwa mfano, nenda kafuatilie (mtandaoni) vitabu vya waandishi kama vile *Kenneth E Haggin na Norvel Hayes* 

....vitabu vyao vina kurasa chache (chini ya 50 au 100), lakini vimefanya vizuri sana sokoni (kimauzo) na kubadilisha maisha ya watu wengi sana duniani.

Kwa hiyo, USIOGOPESHWE NA UKUBWA WA VITABU VYA WAANDISHI WENGINE 

....FANYA KILICHO NDANI YA UWEZO WAKO (huku ukiendelea kujiboresha kila Siku).

CHA MUHIMU: Kitabu chako kiwe kinaongelea kitu kimoja mwanzo mpaka mwisho - kitu ambacho mtu akikisoma kitaweza kumtoa hatua moja kwenda nyingine (kumuongezea thamani).

@lacksontungaraza 

@lacksontungaraza 

Ikiwa una Swali lolote,ULIZA.

WhatsApp 0764 79 31 05

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...