Your Basket

Checkout | Shopping Cart
unaweza inuka tena || GetValue

UNAWEZA, INUKA TENA

UNAWEZA, INUKA TENA

Nimekuwa nikitafakari kwa muda mrefu kuhusu hatima ya maisha ya yangu, nawaza vipi utakuwa mwisho wangu, nani atakuwa mwisho wangu!

Lakini hii si hoja ya msingi sana katika maisha, kwa maana kuogopa kesho yako ni kujiandaa kushindwa! Na kuvaa ujasiri pasipo fikra sahihi ni sawa na kujipiga risasi huku ukijilalamikia.

Mambo tunayoyapitia katika maisha leo, kesho ni hutupa matokeo! Hutupa kile tulichopanda. Inawezekana kweli kabisa, unayakabili matokeo ya madhara ya jana yako, inawezekana kabisa kuna namna unaona chozi lako leo kwa sababu ya mambo fulani fulani, lakini nachofahamu ni kwamba kila angulo linakuja na mafunzo na matokeo yake.


Nimeandika kitabu chenye jina la hii mada, UNAWEZA, INUKA TENA! Nikikusudia kukusaidia kuweza kuelewa umuhimu wa kulipa gharama ya kile ulichokifanya leo, huku nikikupa mwangaza wa kuyakabili matokeo kufikia hatua ya kuweza kuinuka tena!


Wewe ni wa thamani kuendelea kulia hapo chini, wewe ni wa thamani kiasi kwamba kushindwa kuyashinda machozi yako ya kila siku inaweza ikawa na maana tofauti na ushujaa.


Thamani yako isitafsiriwe na yale unayaoyapitia, wala usiruhusu mambo ya maisha kuathiri maisha yako mwenyewe.


Mimi rafiki yako.

Wise Dickson

Morogoro, Tanzania

Ratings: (0) Leave a Comment

You must login to post your comment.

Post Posting...