DHAHABU ILIYOJICHA KWENYE MALISHO
Je, unajua kuwa tatizo linalowatesa wafugaji kila mwaka linaweza kuwa chanzo cha utajiri wako? Dhahabu Iliyojificha Kwenye Kilimo cha Malisho ni kitabu kinachofungua macho yako kuona fursa ambayo wengi bado hawajaiona kwenye biashara ya uzalishaji na uuzaji wa fodder na saileji. Kupitia mifano halisi ya Tanzania na mwongozo wa hatua kwa hatua, utajifunza jinsi ya kuanza hata kwa mtaji mdogo, kupata soko la uhakika, na kujenga biashara yenye faida kubwa.Hiki si kitabu cha kusoma tu ni ramani ya kukuongoza kutoka wazo hadi pesa halisi. Kama uko tayari kubadilisha maisha yako kupitia kilimo cha biashara, basi huu ndio muda wako.Usikos e fursa hii nza safari yako ya utajiri leo.
Dhahabu Iliyojificha Kwenye Kilimo cha Malisho ni kitabu cha kipekee kinachofungua macho ya msomaji kuona fursa halisi ya biashara ndani ya sekta ya mifugo nchini Tanzania. Kikiwa kimejengwa juu ya uhalisia wa changamoto ya upungufu wa nchakula cha mifugo, hasa wakati wa kiangazi, kitabu hiki kinaonesha kwa kina jinsi tatizo hilo linavyoweza kubadilishwa kuwa chanzo kikubwa cha kipato kupitia uzalishaji wa malisho (fodder) na saileji (silage).
Ndani ya kitabu hiki, msomaji ataongozwa hatua kwa hatua kuanzia kubadili mtazamo kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo cha biashara, kuchagua mazao sahihi ya nmalisho kama mahindi, napier na mtama, kuandaa shamba, kupanda, kutunza na kuvuna kwa usahihi. Pia kinaeleza kwa undani teknolojia ya kutengeneza saileji bora, mbinu za kuhifadhi bila kupoteza ubora, pamoja na njia za kuepuka makosa nyanayoweza kusababisha hasara. Zaidi ya hapo, kitabu kinatoa mikakati ya masoko, kupanga bei, na jinsi ya kujenga biashara yenye wateja wa kudumu, hadi kufikia hatua ya kupanua uwekezaji na kuwa mwekezaji mkubwa wa malisho.
Kitabu hiki kimeandikwa na Dkt Peter David Kulyakwave (PhD), mtaalamu wa kilimo, nuchambuzi wa data za kilimo (Agricultural Analytics), na maendeleo ya biashara za kilimo (agribusiness). Ana Shahada ya Uzamili ya Usimamizi wa Biashara (MBA– Hons) kutoka Open University of Tanzania na Shahada ya Uzamivu (PhD) katika Agricultural Analytics kutoka Chinese Academy of Agricultural Sciences, Beijing, China. Uzoefu wake wa kitaaluma na kiutafiti umeiwezesha kazi hii kuwa mwongozo wa vitendo unaoweza kutekelezeka.
Kitabu hiki kinafaa kwa vijana wajasiriamali, wafugaji, wakulima, na yeyote anayetafuta fursa mpya ya kipato katika kilimo cha biashara. Ni mwongozo kamili kwa mtu anayetaka kuanza, kukuza, na kufanikiwa katika biashara ya malisho na saileji katika mazingira ya Tanzania.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godius Rweyongeza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza