IJUE BIASHARA KWA KINA
Biashara na uchumi
Kitabu hiki \"IJUE BIASHARA KWA KINA\" mwandishi amekiandika kwa lengo la kufundisha jamii ili kuepukana na changamoto sugu ambazo watu wamekuwa wakikutana nazo katika sekta ya biashara na kuwapelekea wengi biashara zao kudumaa na biashara zingine kufa kabisa .
Kwa hiyo Kitabu hiki kimejikita sana kuelezea vitu vya muhimu kwenye biashara kama vile;-
Maana ya Biashara. Hapa utaelewa nini maana ya neno Biashara. Kwa sababu watu wengi wanaelewa Tu kwamba biashara ni kununua na kuuza kitu ...Nadharia ambayo sio kweli kabisa. Biashara ni kitu kipana sana ,, inahitaji kujifunza Muda wote.
Aina za Biashara. Katika kipengele Hiki utajifunza Aina mbalimbali za Biashara,ili uelewe ni biashara ipi inayokufaa na unayoiweza wewe ili uweze kuanzisha na baada ya muda ifanikiwe.
Mtaji wa biashara. Hapa utaelewa vizuri NI njia zipi uzitumie ili upate mtaji Kwa urahisi
Maswali ya kujiuliza kabla ya kuanzisha biashara.
Mpango wa biashara n.k
Usomapo Hiki kitabu, hautabaki kama ulivyo.