NAILINDA NDOTO YANGU
Nailinda Ndoto Yangu ni kitabu kinachochambua kwa kina tunu ambazo watoto huzaliwa nazo; namna zinavyoweza kugundulika, namna zinavyoweza kufa au kuwafaa watoto wenyewe na jamii kwa ujumla. Tunu hizo ni maono, ndoto, kipaji na kusudi la mtoto hapa duniani.
Je, kuna mtoto asiye na kipaji chochote? Je, unawezaje kuvumbua kipaji cha mtoto? Je, unawezaje kulinda kipaji cha mtoto na kumsaidia kutimiza ndoto zake? Haya ni maswali yaliyojibiwa na kutolewa ufafanuzi ndani ya kitabu. Kitabu hiki kinawakumbusha wazazi na walezi kuhusu tunu hizo za watoto. Lakini je, ni lipi jukumu la mzazi kuhakikisha tunu hizi za mtoto hazififii au kufa kabisa?. Dhima kubwa ya kitabu hiki ni kuamsha ari ya watoto, wazazi na jamii kugundua, kuzilinda na kuzistawisha tunu hizi ili kuwasaidia watoto waweze kunufaika nazo wao wenyewe na jamii kwa ujumla.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza