NCHI YA USAMBARA
Kitabu juu ya NCHI YA USAMBARA: Historia, Utamaduni, Rasilimali na Urithi
Katika shughuli mbalimbali za wenyeji wa Usambara walitumia neno ‘Shi’ kwa lugha ya Kiswahili 'nchi' wakimanisha ardhi ya Usambara. Eneo lote la Usambara lilikua na utawala wa Zumbe liliitwa nchi ‘Shi’, hivyo neno hili halikutumika tu kwa eneo lote la Usambara bali kwa kila eneo lililokuwa chini ya utawala wa Zumbe.
Usambara (au nchi ya Usambara) ni eneo ambalo lina historia ya kipekee ambayo imeweza kurekodiwa kwa njia mbalimbali kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni na baada ya ukoloni katika eneo la Afrika ya Mashariki. Taarifa nyingi kabla ya mwaka utawala wa Wajerumani katika eneo hili zinatokana na masimulizi ya njia ya mdomo ambayo yamesikilizwa na kuweza kurekodiwa na wanahistoria au wamisionari katika karne ya 18 na 19.
Kitabu hiki kimeandikwa katika mfumo ambao unatoa taswira pana ya kihistoria katika eneo lote la Usambara hususani eneo la magharibi linalounda eneo la wilaya ya Lushoto.