Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Ndoto Ya Yatima - GetValue
Biashara & Ujasilimia Mali

NDOTO YA YATIMA

0
0
  • 5
  • 4
  • 3
  • 2
  • 1
Price:
10,000 Tsh.
Added To Cart:
0
Added to shop:
Nov 13, 2025
Product Views:
74
In category:
Sample

Kitabu \\\"NDOTO YA YATIMA\\\" kinatoa elimu kubwa na ya kiwango cha juu kuhusu ndoto, yatima, hazina na thamani ya hazina zilizofichwa ndani ya mtoto. Kitabu hiki ni zana nzuri sana kwa wanafunzi, wanachuo, wanaharakati, walezi, wazazi, viongozi wa taasisi za kidini, viongozi wa umma ngazi zote, na watoto wote walio chini ya uangalizi. Kitabu kinatoa suluhu ya changamoto za watoto yatima. Ni mwongozo mzuri utakaosaidia wadau wa maendeleo ya watoto na ya jamii kwa ujumla.

Kitabu NDOTO YA YATIMA ni kitabu cha kipekee kwani mwandishi ameandika uhalisia wa janga hili kutokana na uzoefu wa kusaidia watoto yatima kwa zaidi ya miaka 20, ni vema jamii ikipate kitabu hiki ili:-

  • Kuzitambua hazina zilizojificha ndani ya watoto yatima na kisha kuona thamani ya hazina hizo. Kupata mbinu za kuwabaini kirahisi watoto yatima wenye ndoto kubwa na zenye thamani kwa ajili ya kuinua taifa.
  • Kinatoa mbinu za kupata fedha za kuweza kuendeshea miradi ya kusaidia watoto yatima, hatimaye kuwa na wafadhili wakubwa ndani ya Taifa. Wale wenye moyo wa kuwasaidia watoto yatima ila wanakosa fedha, basi kitabu hiki kinatoa suluhisho.
  • Watoto ambao wana wazazi watapata maarifa na mbinu na kuchukua tahadhali mapema kabla ya wazazi wao kufariki ili uyatima ukiwafika wajue nini cha kufanya, watajua wamuone nani na waende ofisi gani ili kuzitimiza ndoto zao.
  • Wazazi watahamasika na kuchukua tahadhali au kinga kwa kutumia maarifa na mbinu zilizomo kwenye kitabu hiki ili kuacha mazingira rafiki kwa watoto wao endapo umauti utawapata kabla watoto wao hawajaanza kujitegemea.
  • Kina mbinu na maarifa yatakayo wasaidia Viongozi na Watumishi wa Serikali na Wizara zake watapata kuboresha au kuweka sera na mikakati mipya kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa kwa kutumia mbinu zilizoibuliwa kwenye kitabu hiki ili kuokoa, kuatamia na kulinda kundi kubwa liwe nguvu ya taifa baadaye.
  • Kitabu kimebainisha maadui wa watoto yatima ambao wasipojulikana wataharibu hazina kubwa zilizo ndani ya watoto yatima. Watoto yatima wakisoma kitabu hiki watapata mbinu jinsi ya kuwashinda maadui hao. Pia kitabu kimebainisha marafiki wa watoto yatima, ili yatima wa sasa na yatima wa baadaye waweze kuwatafuta hao marafiki badala ya kubaki wapweke.
  • Kuna shuhuda za kusisimua na halisi zenye kusikitisha, kuliza, kuchekesha na kuelimisha kutoka kwa watoto yatima waliotimiza ndoto zao.
  • Kuleta mabadiliko chanya juu ya mtazamo hasi wa jamii dhidi ya watoto yatima ikiwa ni pamoja na kujua haki, wajibu wa watoto yatima na wajibu wa jamii kwa watoto yatima. Sambamba na hili baraka na thawabu kwa jamii itakayowajali watoto yatima.
  • Kimejaa Mbinu za kuondoa changamoto zinazowakabili watoto yatima pamoja na mbinu za kupunguza ongezeko la watoto yatima mitaani.
  • Kimevumbua aina za watoto yatima, sababu za kuwepo kwa watoto yatima, na jinsi ya kuwapata walipo ili uweze kuwapatia misaada.
  • Kimeonyesha mashirika yanayowasaidia watoto yatima na kujua vituo au makazi ya kulelea watoto yatima na jinsi ya kuondoa changamoto zinazowakabili watoa huduma za watoto yatima.
  • Kimesheheni Mbinu za kuwasaidia watoto yatima wafanyeje ili kutimiza ndoto zao.
  • Ni Mwongozo kwa Walezi wa watoto yatima waliopo kwenye shule za msingi, shule za sekondari, taasisi za kidini, mashirika yasiyo ya kiserikali, ofisi za serikali au umma, kupata uzoefu wa kuwasaidia kuwalea na kuwaelimisha watoto yatima walio chini yao.
  • Kitabu kinaibua Fursa za ajira kwa vijana kupitia mikakati ya kuwahudumia yatima iliyobainishwa kwenye kitabu. Kitabu hiki si tu kuelimisha jamii bali kinatoa hamasa ya kuchukua hatua kufanyiakazi yale yaliyobainishwa kwani yanafaa kuwainua watoto yatima na ndoto zao.

KARIBU TUSOME KITABU NDOTO YA YATIMA UTAKUWA UMESHIRIKI KUMSAIDIA MTOTO YATIMA KUTIMIZA NDOTO YAKE 

More Products On Discount
20,000 Tsh. 15,000 Tsh.
(13)

Sold by: Prophet Pd John

10,000 Tsh. 9,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

40,000 Tsh. 30,000 Tsh.

Sold by: Reward Kimaro

15,000 Tsh. 10,000 Tsh.

Sold by: Lackson Tungaraza

6,000 Tsh. 5,000 Tsh.

Sold by: Godius Rweyongeza

Best Sellers List
Best Seller
1,000 Tsh.
(5.4)

Sold by: Gaston Ngailo

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PASTOR TONY OSBORN

Best Seller
10,000 Tsh.
(69.8)

Sold by: Samuel Macha

Best Seller
3,000 Tsh.
(16.4)

Sold by: ABDULKADIR MASSA

Best Seller
10,000 Tsh.

Sold by: PETER TARIMO

Best Seller
200 Tsh.
(3.6)

Sold by: Gaston Ngailo

GetValue Recommendations
Old is Gold