Siri Za Kustaafu Kwa Furaha
Price:
14,000 Tsh.
Vendor:
Added To Cart:
0
Added to shop:
Jan 04, 2026
Product Views:
44
Sample
Kwa mujibu wa tafiti, wastaafu wengi hukumbwa na misukosuko ya kisaikolojia, kifedha, kiafya na kimaisha; muda mfupi tu baada ya kustaafu. Hii inaonesha kuwa maandalizi kabla ya kustaafu ni muhimu sana. Ukweli, wanaokosa maandalizi huyumba sana, na wengi wao huishi maisha duni uzeeni. Kitabu hiki kinalenga kumjengea msingi imara mtumishi ili anapostaafu, akiwa amechoka kimwili na kiakili, aende kupumzika kwa utulivu katika maisha yaliyobaki.
Kitabu hiki chenye sura 25, kimejaa mifano mingi halisia. Kimeandikwa kwa lengo kuu la kuwapa maarifa wafanyakazi ambao bado wako kazini ili waanze mapema kufanya maandalizi. Wakiwa kazini, wafanyakazi wengi huwa wanasahau kuwa ipo siku wataingia kwenye maisha binafsi, nje ya vyeo na mishahara yao; tena wakiwa wazee! Kwa hiyo huwa hawafanyi chochote, zaidi ya 'kula nchi'. Hata wakilipwa mafao yao wengi huwa hawajui namna bora ya kuyatumia, na wengi, pesa hiyo huisha ndani ya miaka miwili tu, baadaye. Hili likitokea, mfanyakazi aliyeishi kwa 'kujidai', akiwa kazini, ghafla huingia kwenye mateso, uzeeni. Hali hii haipendezi! Kitabu hiki kimekuja ili kuiondoa kadhia hii.