• Call us +255 717 568 861

Your Basket

Checkout | Shopping Cart
Nitatimiza Ndoto Yangu - GetValueInc
Biashara & Ujasilimia Mali

NITATIMIZA NDOTO YANGU

Ratings

Price:
10,000 Tsh.
Vendor:
Num added to cart:
0
Added to shop:
May 13, 2021
In category:
Sample

Pamoja na kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wenye ndoto hapa duniani hali halisi inaonesha kuwa ni asilimia ndogo sana ya watu ambao hutimiza ndoto zao. Marehemu Myles Mnuroe aliwahi kusema kuwa watu wengi wanakufa na uwezo wao (bila kutimiza ndoto zao) na kwamba makaburini ndiko sehemu utakapowakuta wakurugenzi wengi waliokufa na makampuni yao ambayo hayakuwahi kuanzishwa. Makaburini ndiko sehemu pekee utakutana na vipaji vingi ambavyo havikuwahi kutumika. Kitabu hiki kinaeleza jinsi unavyoweza kufikia ndoto yako haijalishi. Kitabu kimesaidia watu wengi kuishi ndoto zao.

Les Brown mzungumzaji mkubwa kule Marekani aliwahi kusema kuwa ili utimize ndoto yako unahitaji kuwa na njaa ya kuitimiza (you need to be hunger) maana mtu mwenye njaa hatulii anatafuta kitu chochote cha kupoza njaa yake. Kama una ndoto lakini huna msukumo wa kuifikia hakika hautaweza kufika pale unapotamani kufika.Ndoto uliyonayo inabidi ikuendeshe(usitulie).

 

“Nitatimiza Ndoto Yangu”

Other products from this category