INUKA
Kitabu hiki kinaeleza mtu anavyoweza kuruka vihunzi vya vikwazo kedekede na hatimaye kufika pale Mungu alipokusudia afike. Kitabu kinatoa mwanga kwenye giza nene.
“Akili kubwa niliyoiona ndani ya Joas nikiwa katika
Jopo la usaili wa kazi yake mwaka 2014 ,leo naiona kwa kina zaidi kila
nikisomapo kitabu cha INUKA .Hakika Amejikita katika kuwaongoza watu kuziona
,kuzijua na kuzitumia fursa zilizopo ,kutumia mazingira yaliyopo kubuni
shughuli ya kipato kuweka watu pamoja ili washirikiane kiuchumi na kuwasimamia
waweze kufikia mafanikio yao .Hakika Joas Ameletwa na Mungu ili watu wainuke
kiuchumi “.
~John J Msonganzila (Mkurugenzi-Tulip General Credit Ltd )
“Nimemfahamu Joas Yunus tangu nikiwa pamoja nae chuoni
chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ,ni mtu ambaye amekuwa na shauku kubwa
kuona vijana wanainuka na kuchukua hatua madhubuti za kuwaletea mafanikio.Nimepata
muda wa kutosha kupitia maandishi yake katika kitabu cha Inuka toleo la kwanza
.Hakika ameandika mambo muhimu sana kwa watu wa rika zote ambao wanataka kuona
mafanikio katika maisha yao.Kama ningeambiwa nitaje baadhi ya vitabu vya
waandishi wa Kiswahili ambavyo vimeandikwa kwa ustadi mkubwa na vyenye uwezo wa
kubadili maisha ya mtu ,hakika nisingeacha kutaja kitabu hiki miongoni mwavyo”
Kelvin
Kitaso (Mkurugenzi-Gracious Printing Press)
“Kupitia kitabu cha INUKA, nimejifunza kushikilia kile
ninachokiamini mpaka nione matokeo bila
kujali mazingira hasa watu wanaonizunguka .Maneno ninayokumbuka ni kuwa huwezi kumzuia kuku kutaga .Ukijiamini
hakuna anayeweza kuzuia mafanikio yako.Pamoja na kusoma vitabu vya waandishi
wengi kama kitabu cha Tenganamba na vitabu vya Shigongo kitabu cha INUKA baada ya kukisoma kimenifanya ninyanyuke kabisa kwenda kuitimiza ndoto yangu “
Christopher
Ndesambulo(Mjasiriamali wa Nafaka –Dar es salaam