MAFISI KATIKA KANISA
KITABU HIKI CA \\\"MAFISI KATIKA KANISA\\\", NI MSAADA KWA KANISA ILI KUWEZA KUPAMBANUA NS KUJUS ESUMINI SMBSO HSESNS NIS NJEMA KANISA. USIKOSE NAKALA YAKO.
Mafisi ni aina ya wanyama waitwao Fisi. Pia na jina la kitabu hiki kinaitwa “Mafisi katika Kanisa”
Nimeweka “Ma” Badala ya “Fisi” Ili kuonyesha msisitizo wa ubaya wa hao Fisiwatu. Ikiwa na maana neno Mafisi ni neno la kukuza jambo. kama Manguruwe, Mang’ombe, Maembe nk. Ikiwa na maana kuna watu ambao hawakutegemewa kuwomo Makanisani lakini wamo.
Kuna watu ambao wamejificha katika kivuli cha imani kutekereza maovu yao. Mafisi ni wanadamu wenye tamaa, wakitafuta njia ya kupata vitu vyao popote vilipo, mtu mwenye roho ya Fisi, kwake kuwa chochote haoni shida. Hata ukimwambia awe mganga wa kienyeji kwake sawa, au mchawi, kwake sawa, awe mlokole kwake sawa, ilimradi tu tamaa ya uloho wake ifanikiwe.
Kitabu hiki kimelenga kuwafichua wahalifu waliojificha ndani ya Makanisa. Kuna wahalifu wengi, ambao wamegundua kuwa, Kanisani ndio sehemu ambayo wakijificha ni vigumu kuonekana. Kadri siku zinavyoenda, na miaka inavyosogea idadi ya mafisi inaongezeka Makanisani. Kitabu hiki kitalisaidia Kanisa na waumini na Watumishi wa Makanisani kuwagundua Mafisi ndani ya Makanisa yao na jinsi ya kuwashughulikia.