
Chuo Cha Fedha
Chuo Cha Fedha
• Kipato ni zao la thamani unayoitoa kwa wengine. Kuongeza kipato chako, ongeza kwanza thamani unayoitoa kwa wengine.
• Akiba ndiyo mbegu yako ya utajiri. Kabla hujafanya matumizi yoyote yale, weka akiba kwanza.
• Dhibiti matumizi yako. Usitumie fedha kabla hujaipata. Tumia fedha baada ya kuipata, ila tumia kwa kufuata bajeti yako.
• Tajiri humtawala masikini, naye akopaye ni mtumwa wake akopeshaye. Hakikisha unaepuka madeni.
• Kufanya biashara bila kuwa na elimu ya fedha ni kuchagua kushindwa.
• Fedha hufanya kazi kwa bidii na uaminifu kwa mtu mwenye busara ambaye ataiwekeza sehemu inayozalisha.
• Misukosuko ya maisha ikija, bima ndiyo itakayokusaidia. Ila kama hutakuwa na bima, misukosuko ikija, utakuwa hatarini.
• Kila safari ina mwanzo wake. Kujenga utajiri, anzia hapo ulipo.