DIWANI YA TAUSI
Diwani ya Tausi ni mkusanyiko wa mashairi mbali mbali ya kiswahili na tamaduni katika lugha ya kikongo, kinaijeria na kiswahili. Mwandishi kwa kushirikiana na watunzi mbalimbali wamewasilisha sanaa hii katika mtindo huu ili kuenzi na kudumisa utamaduni wa Afrika kwa njia ya lugha.
Diwani ya Tausi ni mkusanyiko wa mashairi mbali mbali ya kiswahili na tamaduni katika lugha ya kikongo, kinaijeria na kiswahili. Mwandishi kwa kushirikiana na watunzi mbalimbali wamewasilisha sanaa hii katika mtindo huu ili kuenzi na kudumisa utamaduni wa Afrika kwa njia ya lugha.
Katika Diwani hii Tausi ametumika kama kiashiria cha utamaduni wetu kama ambavyo tumekuwa tukimtunza na kumhifadhi ndege wa aina hii. Sifa anazobeba ni matazamio ya uzuri wa watu katika nyanja zote. Uzuri wa ndege huyu huleta madaha kama mtunzi anavyosema katika shairi la kwanza “MLIMBWENDE WA BUSTANI” katika kibwagizo cha shairi. Rangi tofauti za tausi zimepambwa katika umaridadi wa asili na rangi kuu ikiwa ni dhahabu na zambarau.
Pia mtunzi anazidi kubainisha utulivu uliopo katika taifa la Tanzania moja ya mataifa ya Afrika yenye kudumisha amani na umoja kwa miaka mingi, haya anayaeleza katika shairi la KIJITO CHA UTULIVU akionesha jinsi gani nchi ya Tanzania imekuwa mahali patulivu na kivutio kwa watalii kutokana na vivutio mbali mbali kama ilivyoelezwa katika ubeti wa nne. Katika shairi la KISWAHILI, mtunzi anatoa wito kwa watu kuja kuzungumza Kiswahili kama moja ya lugha ambayo imekuwa sehemu ya utamaduni kwa watu wa Afrika mashariki na sasa kuenea katika maeneo tofauti ya dunia, wakivutiwa na matumizi ya lugha hii. Wito wake ni kuwa “kujeni tuzungumze kiswahili” hivyo wote mnakaribishwa kutumia lugha ya kiswahili katika nyanja mbali mbali kama sehemu ya kutuunganisha kimawasiliano umoja, upendo na mshikamano katika katika nyanja mbalimbali za maisha.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza