
GERALD: Maamuzi Yanayotuangamiza
Gerald – Maamuzi Yanayotuangamiza ni hadithi halisi ya kusisimua inayochambua maisha ya kijana Gerald kutoka kijijini Tairo hadi mtaani, ambako maamuzi mabaya, tamaa ya pesa, starehe na ushawishi wa marafiki vinambadilisha. Kupitia sura mbalimbali, msomaji anashuhudia mabadiliko ya Gerald kutoka kuwa kijana mwenye ndoto hadi mtu anayejifunza kwa njia ngumu.rnHadithi hii ni sehemu ya mpango kabambe wa “BADILI TABIA MAISHANI: HADITHI ASILIA ZA KIAFRIKA”, unaolenga kuibua fikra mpya, kuhamasisha maadili na kuijenga jamii inayojitambua kupitia simulizi zenye mizizi ya Kiafrika. Ni hadithi ya mafundisho, mabadiliko, na matumaini kwa vijana, wazazi, walimu na jamii kwa ujumla.
Katika dunia ya leo inayobadilika kwa kasi, maamuzi ya binadamu yanaendelea kuwa mhimili mkubwa wa mafanikio au maangamizi yao. Hadithi hii ya "GERALD - MAAMUZI YANAYOTUANGAMIZA" inafungua ukurasa wa kutafakari kwa kina juu ya nafasi yetu kama binadamu katika kuchagua njia sahihi au potofu.
Kwa zaidi ya miaka kumi na tano ya kuchunguza maisha halisi ya watu mbalimbali wa Afrika, nimejifunza kuwa sio utajiri, elimu, utanashati wala umaarufu unaoamua hatima ya mtu – bali maamuzi madogo madogo yanayofanyika kila siku. Kupitia hadithi ya Gerald, tunakutana na maisha ya kijana mwenye ndoto kubwa lakini aliyepotea katika mtego wa maamuzi mabaya yaliyoigharimu familia na jamii yake nzima.
Kitabu hiki kimeandaliwa kwa umakini mkubwa ili kuelimisha, kuburudisha na kuhamasisha jamii ya Watanzania na Afrika kwa ujumla, ili kuishi maisha yenye tafakari, busara na maamuzi yanayoleta tija. Ni wito wa kuamka, kutafakari, na kuchagua kwa hekima kila hatua tunayopiga.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa pumzi na uwezo wa kuandika kazi hii. Aidha, shukrani kwa familia yangu pendwa: mke wangu Debora Petro Chacha, watoto wangu wapendwa Agape, Alfa, Anneth na Angel kwa
v | M a g o t i S a r y a
upendo wao usioyumba. Shukrani za pekee pia kwa kaka zangu Yona, Wankuru, Philimoni, Peter, Daudi na Matare; pamoja na rafiki na mwandishi mkongwe wa fikra tunduizi ndugu Denis Mpagaze kwa kunitia moyo na kunielekeza njia katika safari hii ya uandishi.
Karibu tujifunze kupitia maisha ya Gerald, ili tuweze kujiuliza: Je, sisi tunaelekea wapi na kwa maamuzi gani?
SARYA, Magoti
Geita, Tanzania. Aprili, 2025.
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Godfrey Ngaleya