
ISHI UWEZO WAKO
"Sehemu tajiri zaidi hapa duniani siyo kwenye machimbo ya almasi ya Afrika Kusini, siyo kwenye machimbo ya dhahabu ya Amerika ya Kusini, au kwenye visima vya mafuta vya Iraq na Iran wala siyo kwenye akaunti za benki kubwa duniani. Utajiri mkubwa zaidi hapa duniani upo makabarini" Alisema hayati Dr. Myles Munroe aliyekuwa mchungaji na mwandishi wa vitabu.rnrnHii yote ni kwa sababu makaburini kumezikwa ndoto nyingi ambazo hazikutimizwa, maono ambayo hayakuweza kuwekwa katika uhalisia, ugunduzi ambao haukugunduliwa.rnrnMakaburini wamelala watu ambao walikufa na uwezo mkubwa ndani yao, hawa ni watu ambao walikuwa na mawazo makubwa ya kibiashara lakini hawakuyafanyia kazi, walikuwa na uwezo mkubwa wa mziki lakini hawakuimba, walitakiwa kuandika vitabu vizuri lakini hawakuandika.rnrnNi watu ambao walipaswa kuwa viongozi wakubwa wa kuleta mabadiliko kwenye jamii zao lakini hawakuwa, ni watu ambao walikufa huku dunia ikiwadai kwa kuwa hawakutumia uwezo wao kwa ufasaha ama waliondoka wakiwa hawajamaliza kazi waliokuwa wakiifanya hapa duniani.rnrnMatokeo yake wakaacha ombwe kubwa kwenye maeneo ambayo uwezo wao ulipaswa kutumika. Nisingependa kuona na wewe ukiondoka kwenye hii dunia huku ukiacha dunia ikikudai kwa sababu haukuishi uwezo wako wote, ndio maana nikaamua kukuandikia kitabu hiki ambacho kinakupa mwongozo wa mambo ambayo ukiyatambua na kuyazingatia yatakusaidia kuishi uwezo wako kwa viwango vya juu.Sina shaka kwamba kitabu hiki kinaenda kubadilisha kabisa mtazamo wako juu ya uwezo wako na maisha yako kwa ujumla.rnrnKumbuka kuwa, uwezo wako siyo kile ulichokwisha kukifanya bali ni kile ambacho haujakifanya. Pia kila wakati tambua kwamba una nafasi ya kufanya jambo bora zaidi ya lile ulilokwisha kulifanya.rnrnNB: “Kitu hatari zaidi kwenye maisha siyo kifo bali kile kinachokufa ndani yetu angali sisi tunaishi.” Norman Cousins rnrnIshiUwezoWakornrnZakayo Iganja
"Sehemu tajiri zaidi hapa duniani siyo kwenye machimbo ya almasi ya Afrika Kusini, siyo kwenye machimbo ya dhahabu ya Amerika ya Kusini, au kwenye visima vya mafuta vya Iraq na Iran wala siyo kwenye akaunti za benki kubwa duniani. Utajiri mkubwa zaidi hapa duniani upo makabarini"
Alisema hayati Dr. Myles Munroe aliyekuwa mchungaji na mwandishi wa vitabu kutoka nchini Bahamas
Hii yote ni kwa sababu makaburini kumezikwa ndoto nyingi ambazo hazikutimizwa, maono ambayo hayakuweza kuwekwa katika uhalisia, ugunduzi ambao haukuweza kugunduliwa.
Makaburini wamelala watu ambao walikufa na uwezo mkubwa ndani yao, hawa ni watu ambao walikuwa na mawazo makubwa ya kibiashara lakini hawakuyafanyia kazi, walikuwa na uwezo mkubwa wa mziki lakini hawakuimba, walitakiwa kuandika vitabu vizuri lakini hawakuandika.
Ni watu ambao walipaswa kuwa viongozi wakubwa wa kuleta mabadiliko kwenye jamii zao lakini hawakuwa, ni watu ambao walikufa huku dunia ikiwadai kwa kuwa hawakutumia uwezo wao kwa ufasaha ama waliondoka wakiwa hawajamaliza kazi waliokuwa wakiifanya hapa duniani.
Matokeo yake wakaacha ombwe kubwa kwenye maeneo ambayo uwezo wao ulipaswa kutumika.
Nisingependa kuona na wewe ukiondoka kwenye hii dunia huku ukiacha dunia ikikudai kwa sababu haukuishi uwezo wako wote, ndio maana nikaamua kukuandikia kitabu hiki ambacho kinakupa mwongozo wa mambo ambayo ukiyatambua na kuyazingatia yatakusaidia kuishi uwezo wako kwa viwango vya juu.
Sina shaka kwamba kitabu hiki kinaenda kubadilisha kabisa mtazamo wako juu ya uwezo wako na maisha yako kwa ujumla.
Kumbuka kuwa, uwezo wako siyo kile ulichokwisha kukifanya bali ni kile ambacho haujakifanya na unaweza kukifanya.
Pia kila wakati tambua kwamba una nafasi ya kufanya jambo bora zaidi ya lile ulilokwisha kulifanya.
NB: “Kitu hatari zaidi kwenye maisha siyo kifo bali kile kinachokufa ndani yetu angali sisi tunaishi.” Norman Cousins
#BornFullDieEmpty
#IshiUwezoWako
Zakayo Iganja
Sold by: Lackson Tungaraza
Sold by: Lackson Tungaraza